Random Posts

MAMUYA- JAMII NA WADAU WASHIRIKIANE KUWEZESHA WATOTO YATIMA

Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
...........................................................
TAASISI ya kiislamu ya Waliul Asr seminar(WIPAZ)wilayani Kibaha,mkoani Pwani,imeitaka jamii kushirikiana kuwezesha watoto yatima na wale wenye ulemavu ili kupunguza idadi ya watoto hao iliyopo mitaani.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo,Haroun Mamuya ,alieleza hayo,wakati wa mahafali ya wanafunzi waliopo chini ya taasisi hiyo,shule ya awali, darasa la saba, kidato cha nne, mafunzo ya ualimu wa dini (madrasa) na mafunzo ya ualimu wa shule za awali
Alisema kwamba kwasasa kwa kushirikiana baina ya jamii na wadau mbalimbali itasaidia kuwakomboa watoto hao ambao wanakosa kupata kielimu.

 Baadhi ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu,wakiwa kwenye picha ya pamoja na mkurugenzi wa taasisi ya kiislamu Waliul Asr Seminar(WIPAZ)Kibaha,Haroun Mamuya ambapo taasisi hiyo inawalea na kuwasomesha watoto hao wakiwa 200 .

(Picha na Mwamvua Mwinyi)


 Mkurugenzi wa taasisi ya WIPAZ wilayani Kibaha,Haroun Mamuya ,akuzungumza jambo juu ya shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo,Kushoto ni kaimu mkurugenzi wa taasisi hiyo Isabire Marijani.

(Picha na Mwamvua Mwinyi)

Aidha Mamuya alisema taasisi hiyo inawaendeleza kielimu watoto yatima ambapo kwa sasa inasomesha watoto hao 200 na wenye ulemavu zaidi ya watano.

Alisema taasisi ya Waliul Asr ina shirikiana na serikali kupitia kitengo cha ustawi wa jamii,kuwezesha watoto ambao wazazi wao wamefariki na wasiokuwa na uwezo wa kusomesha watoto wao.

Hata hivyo ,Mamuya alielezea wanawatolea hadi asilimia 95 ya ada wanafunzi wanaofaulu kuendelea kidato cha tano ili wanafunzi wengine waweze kujitahidi kitaaluma.


"Tunawatolea hadi asilimia 95 ya ada wanafunzi wale wanaofaulu kuendelea kidato cha tano ili wanafunzi wengine waweze kujitahidi na tunasaidia wasio na uwezo ambao wamepata daraja la kwanza kidato cha nne"alisema Mamuya.
 Makazi na mazingira wanayoishi watoto yatima ambao wanasomeshwa na kulelewa na kituo cha kulelea watoto chini ya taasisi ya kiislamu Waliul Asr seminar(WIPAZ) Kibaha.

Taasisi hiyo pia inatarajia kuchimba visima kumi katika maeneo yenye uhaba wa maji wilayani Kibaha ikiwemo Pangani ,Viziwaziwa,Mbwawa,Pichandege,Kilangalanga,Mlandizi kwa gharama ya sh.mil 50.
Mbali na hayo wanatarajia kuanzisha chuo cha ufundi VETA na cha wauguzi ili kupika vijana watakaoweza kujiajili miaka ya baadae na kuondokana na utegemezi.
Mamuya alieleza kwamba taasisi yao kupitia shule zake kuanzia chekechea hadi vyuo hawabagui wanafunzi kidini wala kiitikadi.
Aliwaomba wadau wa elimu kushirikiana nao kwa ari na mali kusaidia watoto yatima na wasiojiweza waliopo shuleni hapo.
Awali mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Miembe wilayani Kibaha,Joyce Mwakembe,ambae alikuwa ni mgeni rasmi alisema kuwa kujifunza kwa waliofanikiwa ndiyo siri ya watu wengi.
Alisema mafanikio yanatokana na kuiga yale yaliyofanywa na watu wenye mafanikio na ni chachu kwa wale wanaotafuta maisha.

Post a Comment

0 Comments