Random Posts

MZEE WA BARAZA (64) AHUKUMIWA MIAKA 3 JELA KWA KOSA LA KUOMBA RUSHWA

Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
.....................................................................
MAHAKAMA ya hakimu mkazi wilaya ya Kibaha mkoani Pwani imemuhukumu mzee wa baraza katika mahakama ya mwanzo,Fransis Issaya (64) kwenda jela miaka mitatu ama kulipa faini ya sh.500,000 baada ya kukutwa na hatia ya kupokea na kuomba rushwa.
Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi Harieth Mwailolo alisema mahakama hiyo imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa jamhuri na hivyo anatoa adhabu hiyo ili iwe fundisho.
Awali mwendesha mashitaka wa Takukuru Sabina Weston aliieleza mahakama hiyo kuwa mzee huyo wa baraza alitenda kosa hilo mwezi novemba mwaka huu ambapo alimshawishi Omary Hiza ampe kiasi cha sh.100,000.
Omary aliombwa fedha hiyo ili aweze kusaidiwa mkewe Mariam Hussein aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya jinai 329/2016 kosa la shambulio la kudhuru mwili.
“Ndipo Omary alipoamua kutoa taarifa kwa maofisa wa Takukuru na ambapo mzee huyo alikamatwa baada ya kuwekewa mtego wa wa fedha za moto na kuzipokea kutoka kwa Omary”alisema.
Katika hatua nyingine mkazi wa Kwamatias huko Kibaha,Abduly Omar (27)amehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kujaribu kubaka.
Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi wa mahakama ya hakimu mkazi wilayani hapo,Aziza Mbadyo,alieleza mahakama kuwa imeridhika na ushahidi uliowasilishwa kwenye mahakama hiyo usio na shaka yoyote .
Mwendesha mashitaka wa serikali Lulu Ukwaju alisema mnamo july 7 ,2016 huko Kwamatias Abduly Omar alijaribu kumbaka binti ambae jina linahifadhiwa kwasasa na kabla ya kutekeleza azma yake alikurupushwa na wananchi.

Post a Comment

0 Comments