Random Posts

MATUKIO KATIKA PICHA SHEREHE ZA MIAKA 55 YA UHURU

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akisalimiana na Waziri wa  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,BungeKazi,Ajira,Vijana na Wenyeulemavu Jenister Muhagama mara alipowasili katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kushiriki nkatika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara zilizofanyika leo,mgeni rasmi akiwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli,
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na  Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Mohamed Chende Othman mara alipowasili katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kushiriki nkatika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara zilizofanyika leo,mgeni rasmi akiwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Majaliwa Kassim Majaliwa katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara zilizofanyika leo,ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli
 Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wakati alipoingia katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kuhudhuria katika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara zilizofanyika leo akiwa mgeni rasmi katika sherehe hizo zilizohudhuria na Wnanchi na wageni mbali mbali na Viongozi
Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli (katikati) akifuatana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Devis Mwamunyange baada ya kukagua gwaride maalum la Vikosi vya Ulinzi na Usalama  katika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
[Picha na Ikulu.] 09/12/2016.

Post a Comment

0 Comments