Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Zanzibar Dkt. Amina Abdulkadir
akitiliana saini na Mkurugenzi Mtendaji wa Milele Zanzibar Foundation Yusouf
Luiz mkataba wa maridhiano ya kuimarisha
huduma za Afya vijijini kupitia mradi wa Champion in Health.
Mratibu wa Milele Zanzibar Foundation Ali Bakari Amani akitoa maelezo ya Mradi
wa Champion in Health utakavyowasaidia wanafunzi watakaojiunga na mradi huo
katika kipindi cha miaka mitatu wakati wa utiaji saini katika Chuo cha Taaluma
za Sayansi za Afya kiliopo Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Baadhi ya wanachama wa Champion in Health wakifuatilia utiaji saini mkataba wa
maridhiano kati ya Milele Zanzibar Foundation na Chuo cha Taaluma za Sayansi za
Afya Zanzibar katika sherehe zilizofanyika Chuoni Mbweni nje kidogo ya mji wa
Zanzibar.
Picha ya pamoja ya viongozi wa Milele Zanzibar Foundation na Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya
Zanzibar na baadhi ya wanafunzi watakaofaidika na mradi wa Champion in Health
baada ya sherehe za utiaji saini kumalizika katika chuo hicho.
Picha na
Makame Mshenga.
......................................................................................................
Na Ramadhani
Ali/Maelezo Zanzibar
Milele
Zanzibar Foundation imetiliana saini mkataba wa maridhiano na Chuo cha Taaluma
za Sayansi za Afya Zanzibar mradi wa kuboresha kiwango cha ubora wa utoaji wa
huduma za afya katika maeneo ya vijijini.
Mradi huo wa
miaka mitatu ujulikanao kwa jina la Champion in Health utaangalia changamoto
za Afya vijijini ambako kunaupungufu mkubwa
wa wafanyakazi kutokana na vijana wengi
kukosa hamu ya kufanyakazi katika maeneo
hayo.
Akizungumza
wakati wa kutia saini mradi huo katika Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya
Mbweni, Mratibu wa Milelele Foundation Zanzibar Ali Bakari Amani alisema vijana
98 wakiwemo waliomaliza masomo mwaka huu 2016 na wengine wanaoendelea na masomo
Chuoni hapo watafaidika.
Aliyataja
masharti ya wanafunzi kuingia katika
mradi huo kuwa ni wale waliofanya vizuri
katika masomo, wawe tayari kufanya kazi
vijijini baada ya kumaliza masomo na wazee wawe hawana uwezo wa kuwasomesha.
Ameyataja maeneo makuu ya Mradi kuwa ni kuwapatia
nafasi za masomo nje ya nchi wanafunzi walioteuliwa kuingia katika mradi,
kuwaendeleza na kuwajengea uwezo.
Kaimu Mkuu
wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Zanzibar Dkt. Amina Abdulkadir amewataka
wanafunzi walioingia katika maradi huo kuutumia vizuri msaada huo na
amewashauri kufuata sharti la kuwa tayari kufanya kazi sehemu yeyote watakayo
pangiwa.
Mkurugenzi
Kinga na Elimu ya Afya Dkt Fadhil Abdalla aliipongeza Milele Zanzibar
Foundation kwa kuangali changamoto zinazoikabili jamii hasa vijijini na
kuzitafutia ufumbuzi unaofaa.
Amesema
Wizara hivi sasa inatilia mkazo kuimarisha ubora wa utoaji huduma vijijini
baada ya maeneo mengi kuwa na vituo vya afya na Milele Zanzibar Foundation
imekuwa ikitoa msukumo mkubwa katika sula hilo tokea kuanzishwa kwake miaka
minne iliyopita.
Mradi wa
Champion in Health umetiwa saini na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi
za Afya Zanzibar DKT. Amina Abdulkari na Mkurugenzi Muendeshaji wa Milele
Zanzibar Foundation Yusouf Luiz Caires.




0 Comments