Wafanyakazi wa TBL wakipanda miti katika moja ya kampeni ya upandaji miti.
.......................................................................................................
Kiwanda cha TBL cha Mwanza kimeunga mkono kampeni ya kupanda miti inayoendelea mkoani
Mwanza ambapo kimetoa miche 2,000 ya miti pia wafanyakazi wake wameungana na
viongozi wa serikali na wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za kiserikali na
zisizo za kiserikali kupanda miti katika eneo la Chuo cha Uvuvi .
Meneja Mwandamizi wa TBL,Mwanza,Joseph Malibe, alisema
kuwa kampuni imeunga mkono jitihada hizi ikiwa ni moja ya utekelezaji malengo ya
kampuni ya kulipa suala la mazingira kipaumbele popote inapofanyia biashara
zake pia inayo sera ya sera ya wafanyakazi kutumia muda wao kwa ajili ya kazi
za kijamii.
“Tunafurahi kushiriki
katika tukio hili la kupanda miti lililoandaliwa na taasisi ya mazingira ya
Tanzania Environmental Conservation Organization (TECO) kwa kuwa linaendana na
mtazamo wetu wa kutunza mazingira na vyanzo vya maji”.Alisema Joseph Malibe.
Alisema kuwa TBL itaendelea kuunga mkono jitihada za
utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji popote inapoendeshea biashara zake
ikiwemo kufanya uzalishaji usio na athari
kwa mazingira.
Malibe alisema uzalishaji wa kutumia nishati mbadala tayari
unatekelezwa katika viwanda mbalimbali vya TBL “Hapa Mwanza tumeanza kufanya
uzalishaji kwa kutumia mitambo inayotumia nishati inayotokana na mashudu ya
pamba na pumba za mpunga na katika kiwanda cha Mbeya kimeanza kufanya
uzalishaji kwa kutumia umeme wa nishati ya jua”.
Alimalizia kwa kutoa wito kwa watanzania wote kujenga
utamaduni wa kutunza mazingira ili kupunguza athari kubwa zinazoendelea
kujitokeza sehemu mbalimbali duniani kutokana na uharibifu wa mazingira.

0 Comments