Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Hamad Massauni akisalimiana na wachezaji
wa timu ya watoto kutoka shule ya IST ya jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa
mgeni rasmi katika michezo ya hisani iliyoandaliwa na klabu ya Gymkhana jana
ikiwa na lengo la kusaidia kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park cha
jijini Dar es Salaam .
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Mchezaji
wa timu ya watoto kutoka shule ya IST,
Jack Jere (kushoto) akijaribu kumtoka
Mohamed Mchamungu wa timu ya watoto wa kituo cha Dar es Salaam Academy wakati
wa michezo ya hisani iliyoandaliwa na
klabu ya Gymkhana ikiwa na lengo la kusaidia kituo cha michezo cha Jakaya
Mrisho Kikwete Park cha jijini Dar es Salaam .
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Hamad Massauni (katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya watoto kutoka shule ya IST (wenye jezi
za blue) na timu ya watoto wa kituo cha Dar es Salaam Academy (wenye jezi
nyeusi) kabla ya mchezo wao wakati
alipokuwa mgeni rasmi katika michezo ya hisani iliyoandaliwa na klabu ya Gymkhana
jana ikiwa na lengo la kusaidia kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete
Park cha jijini Dar es Salaam .
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Hamad Massauni akimkabidhi kombe la
ushindi nahodha wa timu ya watoto wa kituo cha Dar es Salaam Academy baada ya
kuibuka mabigwa katika michezo ya hisani
iliyoandaliwa na klabu ya Gymkhana jana ikiwa na lengo la kusaidia kituo cha
michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park cha jijini Dar es Salaam
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Hamad Massauni akikabidhiwa zawadi na
Katibu wa Klabu ya Gymkhana ya jijini Dar es Salaam Khalal Rashid wakati
alipokuwa mgeni rasmi katika michezo ya hisani iliyoandaliwa na klabu hiyo jana
ikiwa na lengo la kusaidia kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park cha
jijini Dar es Salaam
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Hamad Massauni akizungumza na Mkurugenzi
wa ufundi wa kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park cha jijini Dar es
Salaam Bw. Ray Power wakati alipokuwa mgeni rasmi katika michezo ya hisani
iliyoandaliwa na klabu ya Gymkhana
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Hamad Massauni (mwenye jezi nyekundu
aliyesimama) akiwa katika picha ya pamoja na timu ya maveterani ya
Gymkhana Dar es Salaam wakati alipokuwa
mgeni rasmi katika michezo ya hisani iliyoandaliwa na klabu ya Gymkhana kwa
ajili ya kuchangia kituo cha michezo Jakaya Mrisho Kikwete Park cha jijini Dar
es Salaam .
......................................................................................................
Na
Frank Geofray-Jeshi la Polisi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Hamad Massaun amewahimiza viajana nchini
kushiriki michezo ili kuinua vipaji vitakavyowezesha Tanzania kupata wachezaji
wazuri watakaoliwakilisha vyema taifa katika michezo ya kimataifa.
Massaun
alitoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa mgeni rasmi katika kilele cha michezo
ya hisani iliyoandaliwa na klabu ya Gymkhana ya jijini Dar Es Salaam kwa lengo
la kusaidia kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park ambacho kinahudumia vijana katika michezo
mbalimbali.
Massaun alisema ikiwa
wazazi watawasimamia vyema watoto wao katika michezo tangu wakiwa wadogo basi
hapo baadaye nchi yetu itakuwa na wachezaji wengi ambao wataiwakilisha vyema
nchi katika masdhindano mbalimbali.
“Katika nchi nyingine
wachezaji wakubwa hawakuibukia ukubwani, walianza kujiimarisha tangu udogo wao
na ndio maana wanafanya vizuri hivyo na sisi tujielekeze huko ili tuwe na wachezaji bora kama wao na serikali
itaendelea kutoa msaada wa kila aina unaohitajika ili kufanisha azma hiyo ”
Alisema Massaun.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Ufundi wa Kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park Bw.
Ray Power alisema misaada itakayopatikana kutokana na michezo hiyo ya hisani
itatumika kuwaendeleza vijana wadogo waliopo katika kituo hicho ambacho
kimejumuisha michezo mbalimbali.
Katika kilele hicho
Naibu Waziri Massaun alitoa zawadi mbalimbali kwa washindi katika michezo
tofauti iliyoshirikishwa ikiwemo mpira wa miguu, tenesi, magongo na gofu.







0 Comments