Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt. Agustine
Mahiga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu msaada wa dola za Kimarekani
50,000/= sawa na shilingi milioni 108 za Kitanzania zilizotolewa na Balozi wa
Jamhuri ya Korea nchini Bw. Song, Geum-young leo jijini Dar es Salaam. Msaada
huo umetalewa kwa ajili ya kusaidia kurejesha miundombinu na makazi
yaliyoathiriwa na Tetemeko la ardhi Mkoani Kagera mnamo tarehe 9 septemba 2016.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt. Agustine
Mahiga (kulia) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya dola za Kimarekani
50,000/= sawa na shilingi milioni 108 za Kitanzania zilizotolewa na Balozi wa
Jamhuri ya Korea nchini Bw. Song, Geum-young leo jijini Dar es Salaam. Msaada
huo umetalewa kwa ajili ya kusaidia kurejesha miundombinu na makazi
yaliyoathiriwa na Tetemeko la ardhi Mkoani Kagera mnamo tarehe 9 septemba 2016
Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Balozi Dkt. Agustine Mahiga (kushoto) akiagana na Balozi wa Jamhuri ya
Korea nchini Bw. Song, Geum-young mara baada ya kupokea msaada wa Dola za Kimarekani
50,000 leo jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetalewa kwa ajili ya kusaidia
kurejesha miundombinu na makazi yaliyoathiriwa na Tetemeko la ardhi Mkoani
Kagera mnamo tarehe 9 septemba 2016.
Picha na MAELEZO.
.............................................................................................................................
Na: Frank Shija –
MAELEZO.
27/12/2016
Tanzania yadhamiria
kuimarisha uhusiano baina yake na Jamhuri ya Korea kwa kufungua Ofisi zake za
Ubalozi Mjini Seoul, nchini Korea.
Hayo yamebainishwa na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine
Mahiga leo jijini Dar es Salaam wakati akipokea msaada wa Dola za Kimarekani
50,000 kwa ajili ya kusaidia urejeshaji wa miundombinu iliyoharibika kutokana
na Tetemeko la Ardhi lilitokea Mkoani Kagera mnamo tarehe 9 Septemba 2016.
Balozi Mahiga amesema
kuwa nchi ya Jamhuri ya Korea imekuwa na uhusiano mzuri na wa muda mrefu na
Tanzania ambapo kupitia uhusiano huo imekuwa ikisaidia katika mambo mbalimbali
ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya afya akitolea mfano Hospitali za
Mloganzila na Chanika ambazo zote zimejengwa kwa ufadhili wa Shirika la Kimataifa
la Mahusiano la Korea (KOICA).
“Korea imekuwa na Ofisi
za Ubalozi hapa nchini kwa zaidi ya miaka 25 hivyo wameona ni wakati sasa kwa
Tanzania kuwa na Ofisi yake Ubalozi nchini nnchini Korea,” Alisema Balozi
Mahiga.
Kwa upande wake Balozi
wa Jamhuri ya Korea nchini Bw. Song, Geum – Young amesema kuwa msaada huo
unatokana na namna ambavyo waliguswa na janga la Tetemeko la ardhi lililotokea
Mkoani Kagera na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu na makazi ya
wananchi.
Ameongeza kuwa msaada
huo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi aliyoitoa kwa Rais Dkt. Magufuli
alipomtembelea Ikulu na kumpa Pole mnamo tarehe 22 Septemba mwaka huu.
Balozi Song Geum-Young
pia amemhakikishia Waziri Mahiga kuwa Korea itaendeleza na kuimarisha uhusiano
wake na Tanzania na kwamba itatoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha miradi ya
maendeleo ambayo inatekelezwa hapa nchini ikiwemo ujenzi wa Daraja la Salender,
Meli, Hospitali ya Mloganzila, Chanika na mingineyo.
No comments:
Post a Comment