Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa akisalimiana na Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Alhaj Abukary Zubeiry Bin Ally baada ya kuwasili
Shelui mkoani Singida kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Maulid Desemba 12,
2016. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi.
(Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri
wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba baada ya kuwasili Shelui
mkoani Singida kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Maulid Desemba 12,
2016. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Rais, January Makamba.
Muungano na Mazingira,
Baadhi ya washiriki wa Baraza la Maulid wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
wakati alipohutubia Baraza hilo , Shelui
mkoani Singida, Desemba 12, 2016.
Waziri wa
Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akizungumza katika Baraza la Maulid lililofanyika Shelui mkoani Singida ambapo mgeni rasmi
alikuwa ni Waziri Mkuu, Kassim Majalaiwa , Desemba 12, 2016.
Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania,
Alhaj Abubakary Zubeiry bin Ally akizungumza katika Baraza la Maulid
lililofanyika kitaifa Shelui mkoani
Singida na mgeni rasmi alikuwa ni Waziri Mkuu, Kassim Majliwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Baraza la Maulid
lililofanyika kitaifa, Shelui, Singida
Desemba 12, 2016..
Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi
baada ya kuwasili Shelui kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Maulid, Desemba 12, 2016.
.................................................................................................................................
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewataka viongozi wa dini nchini kutimiza wajibu wao kwa kuwahimiza waumini
wao kujiepusha na kauli na vitendo vitakavyopandikiza chuki na uchochezi miongoni
mwa waumini wa dini moja na waumini wa dini nyingine .
Ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu ,
Desemba 12, 2016) wakati akihutubia kwenye baraza la Maulid lililofanyika
Shelui mkoani Singida, ambapo amesisitiza kwamba Serikali ya awamu ya tano ipo
imara na haitayumba .
"Ni vyema tukatambua kwamba
katika mifarakano na uhasama wa kidini hakuna atakayeibuka mshindi bali wote
tutakuwa ni watu tulioshindwa . Nyumba za ibada zisaidie kuunganisha waumini na
kuwa mfano usoni kwa jamii ,"
Amesema mara kadhaa watu
wameshuhudia migogoro na mapigano kwenye Misikiti wakigombea uongozi na mali
matukio ambayo hayana tija ndani ya Uislam, hivyo ni vyema wakafuata misingi ya
dini ya kuheshimiana , kuelewana na kuvumiliana. Watumie mabaraza kukemea hali
hiyo inayowagawa Waislam .
Amesema Serikali itaendelea
kuzitegemea dini zote nchini kujenga msingi imara wa kuleta amani
miongoni mwa Watanzania. Serikali itaendelea kusisitiza na kuheshimu
uhuru wa raia wa Tanzania kuabudu dini wanayoiamini kwa sababu ni moja kati ya
haki za msingi za kila mwananchi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya
muungano wa Tanzania
"Napenda kuwahakikishia kwamba
Serikali itaendelea kufanya kila iwezalo kuhakikisha kwamba uhuru huo
unaheshimiwa . Hii ni nyenzo muhimu iliyosaidia kulifanya Taifa letu kuwa ni
mfano wa kuigwa kote ulimwenguni .Tutaendelea kushirikiana na viongozi wa dini
zote nchini ili kuhakikisha kuwa tunu hiyo muhimu haichezewi na mtu au kikundi
chochote," amesema .
Wakati huo huo, Waziri Mkuu
alizungumzia suala la kuwepo kwa tishio la ugaidi duniani ambalo limegharimu
maisha ya baadhi ya wananchi." Aidha , mmezungumzia kuhusu uwezekano wa
baadhi ya watuhumiwa wa ugaidi kufunguliwa mashtaka kwa sababu ya chuki au
kulipiza kisasi,”.
“Napenda kuwahakikishia kwamba
Serikali iko macho katika kupambana na tishio lolote la kiusalama ndani na lnje
ya mipaka ya nchi yetu. Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama viko katika hali ya
utayari wakati wote ili kupambana na vikundi au watu na mtu yeyote mwenye nia
ya kuhatarisha usalama wa nchi yetu,” amesema.
Hata hivyo, Waziri Mkuu ametumia
fursa hiyo kuwakukumbusha viongozi wa dini kwamba jukumu la ulinzi wa nchi yetu kwa
mujibu wa Katiba ni jukumu la kila mwananchi. “ Yaani kila Mtanzania,".
Waziri Mkuu ameongeza kuwa ni vyema
viongozi wa dini wakatambua kwamba wao pamoja na waumini wanaowaongoza ndio
walinzi wa Taifa hivyo wanalo jukumu la kuendelea kuwasihi waumini kuendelea
kuwa raia wema na kutoa taarifa za dalili za uhalifu mapema iwezekanavyo .
"Mathalan , hawa watoto
wanaojiita panya road huko Dar es Salaam au vijana wanaoteka magari pale mlima
Sekenke , hawatoki kwenye sayari nyingine ni watoto wetu tunaishi nao majumbani
, tunaabudu nao Misikitini au Makanisani. Ni jukumu la kila mmoja wetu
kuwaripoti kwenye vyombo vya ulinzi na usalama ili watambulike na
washughulikiwe ipasavyo. Wasiendelee kuleta madhara kwa raia wema ,"
amesema .
Kwa upande wake Mufti na Sheikh Mkuu
wa Tanzania Aboubakar Bin Zuber amewasihi waislam nchini kuishi
maisha ya Mtume Muhammad (SWA) ambaye alisisitiza kupendana na kushikamana
,kuwajali wengine bila kuwabagua kiimani ,kupenda kufanya kazi halali na
kujifunza.
“Si jambo rahisi kupata kipato bila
kufanya kazi ,tutalaumu kila siku kuwa hatuoni mabadiliko ya kipato wakati sisi
wenyewe hatufanyi kazi. Uislam ni kielelezo tosha kwa mfano wa maisha bora, si
kweli kuwa dini yetu inafundisha tuchukie wengine,” amesisitiza.
Pia Sheikh Zubeiry amewaasa
waumini wa dini zote kushika imani iliyosahihi huku akiwaomba kupuuza kauli za badhi ya watu kudai magaidi
hutokea katika dini ya kiislam kutokana kuwa na imani kubwa ya kiislam.
Kwa upande wake Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba amesisitiza kupambana na
watu ambao wamekuwa wakienda kinyume na sheria za nchi.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, DESEMBA 12, 2016.



0 Comments