Mwenyekiti wa wa jumuiya ya Singasinga( Guru Singh) akimkabidhi madawati mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ikiwa ni sehemu ya mchango wa jumuiya hiyo kukabiliana na tatizo la upungufu wa madawati kwa shule ya sekondari Kiwangwa wilayani Bagamoyo .
(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Katibu wa Jumuiya Singasinga (Guru Singh)Jasdeep Singh Babrah akiteta jambo na mbunge wa jimbo la Chalinze Roidhiwani Kikwete mara baada ya kumaliza zoezi la kukabidhi madawati 100 yenye thamani ya sh.mil tano,kwa shule ya sekondari Kiwangwa wilayani Bagamoyo,kushoto ni mkuu wa wilaya hiyo Alhaji Majid Mwanga,na Diwani wa Kata ya Kiwangwa Malota Kwaga .
(picha na Mwamvua Mwinyi)
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Alhaji Majid Mwanga,akipanda mti katika shule ya sekondari Kiwangwa ikiwa ni sehemu ya kukamilisha zoezi la kuhamasisha wakazi wa wilaya hiyo kupanda miti ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na ukame.
(Picha Mwamvua Mwinyi)
..........................................................................................
Na Mwamvua Mwinyi, Kiwangwa
Jumuiya ya Singh maarufu kama masingasinga hapa nchini imetoa msaada wa madawati 100 na meza 100 ,vyenye gharama ya mil. 5,kwa shule ya sekondari ya kata ya Kiwangwa,chalinze wilaya ya Bagamoyo.
Jumuiya hiyo imetoa msaada huo ,ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha sekta ya elimu.
Akiongea kwa niaba ya mwenyekiti wa Jumuiya hiyo,Kurgis,katibu wa Jumuiya hiyo ya Singh bw .Singh alisema ubora wa upatikanaji wa elimu katika shule unategemea mchango wa kila mdau hivyo wao wameamua kuanza na madawati .
Alisema lengo ni kuhakikisha watoto wanasoma kwenye mazingira mazuri na hatimae kutimiza ndoto zao.
,”Ndugu zangu sisi Singasinga tumeamua kuanza na madawati lengo letu ni kuona watoto wakisoma katika mazingira rafiki,hatimae waweze kufika mbali kielimu”alisema Kurgis .
Akizungumza katika hafla ya upokeaji wa madawati hayo mgeni rasmi, mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete,aliishukuru jumuiya ya Singasinga kwa msaada huo na kusema utasaidia watoto kuondokana na adha ya kukaa chini .
”Ndugu yangu Kurgis mmetufaa sana kwakweli,lakini tunawaomba msituchoke. Changamoto ziko nyingi sana katika maeneo yetu."
" Leo tunawashukuru kwa madawati lakini tatizo la maji na umbali wa wanapoenda kuchukua maji vijana wetu unasababisha pia kushuka kwa viwango vya ufaulu sio tu shuleni hapa lakini katika maeneo mengi ndani ya halmashauri yetu.alieleza Ridhiwani.
Ridhiwani aliwaomba wajaribu kusaidia changamoto hiyo kwa kuiweka kwenye mipango yao kazi ya maendeleo ya jamii.
Alifafanua endapo jumuiya hiyo itasaidia kuchimba visima italeta tija katika maeneo mengi jimboni hapo maana pia watoto wanateseka kutokana shule nyingi hazina huduma ya maji.
Ridhiwani alisema kijumla Jimbo hilo limeshakamilisha kutatua tatizo la upungufu wa madawati na wanashukuru kupata ya ziada.
Mbunge huyo alisema kwasasa nguvu zao zinaelekezwa katika ujenzi wa madarasa mashuleni na kukarabati yale chakavu hivyo aliwaomba wadau wa maendeleo wajitokeze kuunga mkono suala hill.
Nae diwani wa kata ya Kiwangwa Malota Hussein Kwaga, ambae ndie aliyefanikisha kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa madawati hayo alitoa wito kwa walimu na wanafunzi kuhakikisha wanayatunza madawati hayo ili yaweze kutumika kwa kipindi kirefu .
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Alhaj Majid Mwanga, alimpongeza diwani huyo kwa hatua nzuri anazozifanya za kuwasaidia wananchi wake na sio kuangalia kuneemeka yeye binafsi.
Alisema ni mfano mzuri wa kuigwa katika halmashauri hiyo.
Shule ya sekondari Kiwangwa ilianzishwa mwaka 2004,tangu kuanzishwa kwake imekuwa inategemea misaada mbalimbali ili kufikia malengo waliyoanzisha.
No comments:
Post a Comment