Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni, akipokea salamu za heshima baada ya kuwasili kituo cha
Uhamiaji Kasumulu, kinachosimamia masuala ya uingiaji na utokaji nchini kwa
wananchi wa Nchi za Tanzania na Malawi. Kulia ni Afisa Uhamiaji Mfawidhi wa
kituo hicho, Kamishna Msaidizi Taniel Magwaza. Naibu Waziri yupo wilayani Kyela
kwa ziara ya kikazi.
(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni (kushoto),
akikagua hati ya kusafiria ya mwananchi kutoka nchi ya Malawi, Miston
Chikankheni aliyekuwa anaingia nchini
katika Kituo cha Uhamiaji Kasumulu, wilayani Kyela mkoa wa Mbeya. Naibu Waziri
yupo wilayani Kyela kwa ziara ya kikazi.
(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
MraKibu Mwandamizi wa Idara ya Uhamiaji, Gragiza
John akijibu maswali aliyoulizwa na
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili
kushoto) ,baada ya kutembelea moja ya vipenyo vinavyopitisha wahamiaji haramu
kutoka Malawi katika mpaka wa Kasumulu. Naibu Waziri ameiagiza idara hiyo wakishirikiana na Jeshi la Polisi kudhibiti
njia hizo ili kuzuia uingiaji wa wahamiaji hao, wakati wa ziara ya kikazi wilayani
Kyela.
(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni,akumuuliza swali, Mrakibu Mwandamizi wa Idara ya
Uhamiaji, Gragiza John(kulia) wakati wa
ziara yake ya kikazi ya ukaguzi wa vipenyo vinavyotumiwa na wahamiaji haramu
mpakani Kasumulu kuingia nchini wakitokea Malawi. Naibu Waziri yupo wilayani
Kyela kwa ziara ya kikazi. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji jijini Mbeya, Kamishna
Msaidizi, Asumsio Achachaa, akizungumza na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) baada ya kutembelea mpaka waKasumulu
unaotenganisha nchi za Tanzania na
Malawi wilayani Kyela. Mlima unaoonekana nyuma upo nchini Malawi. Naibu Waziri yupo wilayani Kyela kwa
ziara ya kikazi.
(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Afisa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Lenny Mkola, akijibu swali lililoulizwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni linalohusiana na mapato kwenye mpaka wa Kasumulu unaotenganisha nchi
za Tanzania na Malawi. Naibu Waziri yupo wilayani Kyela kwa ziara ya kikazi.
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI- WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI






0 Comments