Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Angellah J. Kairuki na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro wakiuaga msafara wa
magari yaliyobeba vifaa
vya ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo leo Jijini Dar es
Salaam wakielekea Dodoma kwenye makao makuu ya nchi.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Angellah J. Kairuki akizungumza na watumishi wa ofisi yake juu ya safari ya
kuhamia Dodoma iliyoanza rasmi leo kwa kuhamisha vifaa vya ofisi vya kundi la
kwanza la watumishi wa ofisi hiyo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Angellah J. Kairuki akizungumza na waandishi wa habari juu ya safari ya kuhamia
Dodoma iliyoanza rasmi leo kwa kuhamisha vifaa vya ofisi vya kundi la kwanza la
watumishi wa ofisi hiyo.Kushoto kwa Waziri ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -Menejimenti ya Utumishi wa
Umma Dkt. Laurean Ndumbaro na Naibu
Katibu Mkuu-Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.
Susan Mlawi.
...............................................................................
Na Daudi Manongi-MAELEZO.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki amezindua rasmi safari ya
awamu ya kwanza kwa kuaga msafara wa magari yaliyobeba vifaa vya Ofisi vya
kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo kuelekea Dodoma.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Kairuki alisema umefika
wakati wafanyakazi wa Serikali kuanza safari ya kuamia makao makuu Dodoma ili
kutimiza ahadi iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John
Pombe Magufuli wakati wa Maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa.
“Kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Waziri
Mkuu kama kiongozi na mratibu wa shughuli za Serikali alihamia Dodoma Mwezi
Septemba 2016,Wizara nyingine zimeendelea na maandalizi ya kutekeleza azma hii
ya serikali, nami leo napenda kutumia fursa hii kuuarifu umma wa watanzania
kuwa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imekamilisha
maandalizi ya kuhamia Dodoma na hivi punde vifaa vya kundi la kwanza vitaondoka
kwenda Dodoma”,Aliongeza Mhe. Kairuki.
Amesema katika kundi la kwanza jumla ya watumishi 87
watahamia Dodoma na litahusisha uongozi
wa Juu wa Wizara ukiwajumuisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu na Baadhi ya
Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi, Maafisa Waandamizi na Watumishi wengine.
Katika hatua nyingine Mh. Kairuki alisema wale wote
wanaohitaji kukutana na Waziri,Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wake wafike
katika Ofisi zilizopo Dodoma na kwa masuala yote yanayohusuu Sera na Sheria za
Utumishi wa Umma na Utawala wa Utumishi wa Umma kwa Ujumla yatatekelezwa Mjini
Dodoma lakini.
Aidha masuala ya Mishahara,Uendelezaji rasilimali
watu,Ukuzaji maadili,Anuai za jamii,Uchambuzi ushauri na Utendaji kazi na Huduma
ya teknolojia ya habari na mawasiliano yataendelea kushughulikiwa na ofisi ya
Dar es Salaam.
Alisema Ofisi yake itafunguliwa
Rasmi Mjini Dodoma Tarehe 30 Januari 2017 na itakuwa katika Jengo la College of
Humanities and Social Sciences katika eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma kama makao
yake ya muda mpaka hapo itakavyoelezwa vinginevyo.



0 Comments