Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemshukuru Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli kwa kuridhia
kufunguliwa tena Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kadhalika,
TFF inamshukuru Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape
Nnauye kwa juhudi zake na kwamba namna aliyoonesha ushirikiano
kufanikisha suala la kufunguliwa uwanja huo uliofungiwa matumizi yake na
Serikali, Oktoba mwaka uliopita.
TFF
inachukua nafasi hii kuahidi kuwa itasimamia matumizi mazuri ya uwanja
huo kwa kutoa elimu kwa wadau ili kuutumia uwanja huo vema ikitambua
kuwa ni hazina ambayo imetokana na nguvu na gharama kubwa za Serikali
kuujenga uwanja huo.
TFF
inatahadharisha mashabiki wa mpira wa miguu kwamba uwanja huo umejengwa
kwa gharama kubwa hivyo ni jukumu letu kuutuza na kuutumia vema kwa
sababu ni hazina kubwa tuliyonayo na ni miongoni mwa urithi bora kwa
vizazi vijavyo.
Kwa
sasa tumetuma maombi yetu Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuomba
kuutumia uwanja huo kwenye mchezo wa kesho Jumamosi Januari 28, mwaka
huu kati Simba na Azam utapigwa kwenye uwanja huo wa Taifa, Dar es
Salaam kadhalika keshokutwa katika mchezo kati ya Young Africans ya Dar
es Salaam na Mwadui ya Shinyanga.
Ratiba
ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inaonesha kuwa ligi hiyo huko
Mbeya kutakuwa na ‘derby’ kwa maana ya mchezo wa upinzani baina ya timu
zinazotoka mkoa mmoja wa Mbeya ambazo ni Tanzania Prisons na Mbeya City
utakaochezwa na Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Keshokutwa
Jumapili Januari 29, mwaka huu kutakuwa na mchezo mwingine ambao Young
Africans itacheza na Mwadui jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam wakati Majimaji ya Songea itasafiri hadi Mtwara kucheza
na Ndanda kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Jumatatu
Januari 30, 2017 kutakuwa na mchezo mwingine kati ya Kagera Sugar na
Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba wakati JKT Ruvu
itakuwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
..………………………………………………………………………… ........................
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

0 Comments