| Diwani wa Kata ya Nyang'oko Elias Ngolle akimwelezea Mkuu wa Mkoa changamoto ambazo zipo kwenye kata yake.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amefanya ziara ya kutembelea vijiji na mitaa katika wilaya ya Geita lengo likiwa ni kuzungumza na kujua wananchi ambao wanapatiwa fedha kutoka kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini awamu ya tatu (TASAF ) wanavyofaidika na fedha hizo na namna ambavyo wamezifanyia kazi na uelewa wa mfuko huo.
Kyunga ametembelea kwenye Kata za Busanda,Nyakamwaga ,Nyan’goko ,Mtakuja na Bumwongoko kubwa akikisitiza wananchi ambao wanapatia fedha hizo kutoka kwenye mfuko wa huo kutumia kwa maendeleo ambayo yatawasaidia hata baada ya kuwa muda umemalizika wa kupatiwa ruzuku.
“Mpango wa kuhudumia kaya masikini ni wa miaka mitatu hadi sasa wamelipwa awamu kumi hivyo wamebakiza awamu nane za kulipwa hivyo nawaomba wananchi kuakikisha
muda uliobaki mnatumia fedha kwa manufaa na kwa Faida zaidi ikiwa ni
pamoja na kununua vitu ambavyo vitawasaidiam kuongeza kipato kwenye familia zenu”Alisema Kyunga.
Hata hivyo baadhi ya wanufaika wa mradi huo wamesema kuwa tangu kuanzishwa wamefaidika na vitu vingi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba pamoja na kusomesha
watoto hivyo kutokana na hatua hiyo wameishukuru serikali kwan maana
imeweza kuwasaidia wale ambao walikuwa awana uwezo.
“Mimi naitwa Valentino Sweya naishukuru sana serikali kwa kuleta mradi huu kwakweli mimi nimenufaika sana kwani nimeweza kujenga nyumba ya chumba kimoja na sebule ,pia nimekuwa nikinunua chakula na pia nimeweza kununua nguo za wanafunzi kiukweli nimenufaika sana na Tasaf”Alisema Sweya.
“Hatujawai kukutana na changamoto yoyote kwenye malipo kwani tumekuwa tukipatiwa fedha kwa msingi mzuri tatizo baadhi yetu awana elimu kabisa ya matumizi ya fedha hizi kwani wamekuwa wakitumia pasipokujua matumizi sahihi ya fedha hizi mimi niombe basi serikali itoe elimu ya kutosha kwa walengwa”alisema Mzee Danile Safari.
Hata
hivyo katika ziara yake ya siku Mbili kwa halmashauri zote mbili za
wilayani GEITA Mkuu wa mkoa wa Geita , amekutana na changamoto ya
wanufaika wa mradi huo kutokujua kikomo cha kupokea fedha na wengine kushindwa kutimiza makusudio ya fedha hizo kama ambavyo zimepangwa kufanya shughuli za kimaendeleo na kunusuru kaya ambazo hazina uwezo wa kifedha na kipato na wale, ambao walishindwa kuwasomesha watoto.
|
0 Comments