Waziri
wa nishati na madini ,Professa Sospeter Muhongo,amemwagiza Kamishina wa
madini kanda ya ziwa kutembelea migodi yote na kuikagua ili kujua hali
ilivyo na kuakikisha wanatoa mashariti katika migodi yote mikubwa,ya
kati na midogo.
Hayo
ameyasema wakati alipowatembelea wachimbaji kumi na tano ambao
walifukiwa na kifusi kwenye mgodi wa RZ union uliopo kwenye kijiji cha
mawemeru Kata ya Nyarugusu wilaya na Mkoa wa Geita.
Prof,Muhongo
amemwagiza kamishina wa madini kuakikisha anafanya ukaguzi na
kutembelea migodi yote na kwamba kufikia tarehe 16 ya mwezi wa tatu awe
ametoa taarifa ya hali ilivyo kwenye migodi ambayo hatakuwa ametembelea.
“Kamishina
nimekwisha waelekeza tembeleeni Migodi yote mkague na kwasababu watu
wanaendelea kuchimba kama nyie ni wachache tuongezeni nguvu kutoka
wizarani,kutoka stamiko,siorojiko au chuo kikuu leo ni tarehe 17 hadi
kufikia 16 mwezi ujao nipewe ripoti ya ukaguzi”Alisisitiza Prof Muhongo.
Kamishina
Msaidizi wa madini kanda ya ziwa victoria magharibi Yahaya Samamba
,amemweleza waziri wa nishati na madini sababu zilizopelekea kuanguka ni
kutokana na kuzidiwa kwa udongo uliokuwa juu pamoja na kuwa ni mgodi wa
muda mrefu hivyo timba zilikuwa zimekwisha anza kuoza na kwamba hatua
ambazo zimechukuliwa hadi sasa ni mgodi kufungwa hadi yale maelekezo
waliyopatiwa yatakapo kuwa yamekamilika.
“Uchunguzi
uliofanyika umeonyesha kuwa mgodi huu umeanguka kutokana na kuzidiwa
na udongo laini juu pia mwamba laini ulioza kiasi cha takribani mita 15
kutoka usawa wa ardhi lakini pia sambamba na hilo mgodi huu una muda
mrefu zaidi ya miaka mitatu kwa hiyo zile sapoti kwa maana ya timba
zilikuwa zimekwisha hanza kuoza na tulikuwa tumekwisha wapo maelekezo
wakati wakiwa kwenye marekebisho ya kuweka chuma ndio ajali hii iliweza
kutokea kazi inayoendelea hivi sasa ni kutoa maji kwenye shimo ili
kuakikisha mazingira yanakuwa mazuri ili kufanya yale ambayo yameagizwa
na kamishina wa madini”Alisema Samamba.
Kwa
upande wake msemaji wa mgodi huo na mwanasheria,Francis Kiganga
,amemwomba Waziri wa nishati na madini kutia sahini ya hati ya
uhamishaji miliki kwa maana pande zote mbili wamekubaliana kwa muuzaji
abaki na asilimia 15 na mnunuzi ahamishiwe asilimia 85.
Hata
hivyo ombi hilo alikukubaliwa na waziri wa nishati na madini hadi pale
mgodi huo utakapokuwa umetimiza mashariti ambayo wamepatiwa.
Hata
hivyo Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl,Herman Kapufi,amemweleza waziri
Muhongo kuwa wamefatilia kuakikisha vijana wanapatiwa mikataba ya
kudumu .
Akizungumza
kwa niaba ya wachimbaji wenzake ambao walinusurika kwenye ajali hiyo
Ansenti Masanja amemshukuru waziri Muhongo kwa kuwatembelea na kuja
kuwajulia hali zao ikiwa ni pamoja na kuwapa pole.
0 Comments