
Kamanda
wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akipokea vifaa vya
kuzuia vumbi kwa askari wa usalama barabarani kutoka kwa msamaria
mwema, Tahir Othman (kulia) ,aliyejitolea vifaa hivyo ili kusaidia
askari kuepukana na vumbi kuingia kwenye njia ya hewa wawapo katika
shughuli zao.Anayeshuhudia katikati ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni .Makabidhiano hayo yamefanyika
ofisini kwa Naibu Waziri,jijini Dar es Salaam.

Kamanda
wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akionyesha kwa
waandishi wa habari jinsi ya kuvaa kifaa cha kuzuia vumbi kwa askari
wa usalama barabarani alivyopokea kutoka kwa msamaria mwema,Tahir
Othman(hayupo pichani) ,aliyejitolea vifaa hivyo ili kusaidia askari
kuepukana na vumbi kuingia kwenye njia ya hewa wawapo katika shughuli
zao.Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi
Hamad Masauni. Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri,
jijini Dar es Salaam.

Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni,
akiangalia jinsi ya kuvaa kifaa cha kuzuia vumbi kwa askari kutoka kwa
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, ambae pia ni
Katibu Mtendaji wa baraza hilo.Vifaa hivyo vilitolewa na msamaria
mwema,Tahir Othman (hayupo pichani).Makabidhiano hayo yamefanyika
ofisini kwa Naibu Waziri,jijini Dar es Salaam.
0 Comments