Hati chafu ni Matokeo YA kutozingatia taratibu za Fedha WANANCHI wanapunguza imani kwa halmashauri zao kupata hati za mashaka
Azikumbusha halmashauri kutenga asilimia 10 YA mapato YA ndani kwa ajili YA mikopo YA wanawake na vijana Mkuu wa Mkoa wa Mbeya leo amekutana na wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wakuu wa idara wa halmashauri zote katika kikao cha kawaida cha kupokea na kupitia taarifa za kudhibiti mapato na matumizi za halmashauri na kuzitaka halmashauri hizo kufuata taratibu za Fedha katika shughuli za kila siku na kufanya hivyo wataepuka kupata hati chafu
Amesema halmashauri inapopata hati chafu wananchi hupunguza imani kwa halmashauri yao hivyo ni vema jitihada za makusudi zifanywe ikiwemo kuzingatia ushauri wa CAG, mkaguzi wa ndani na kufuata taratibu za Fedha kutasaidia kupata hati safi

0 Comments