Fundi wa kuchoma vyuma kwa kutumia teknolojia ya gesi akiendelea na
zoezi la kuchoma kufuli ya lango la ghala lililofichwa kwenye hoteli ya
Butterfly iliyopo mtaa wa Muhonda eneo la Kariakoo. Ghala hilo
limekutwa na shehena kubwa ya kazi haramu za muziki na filamu.
Mmiliki wa ghala lilolokutwa chini ya hoteli ya Butterfly Phili
Ulaya akijaribu kujitetea mbele za Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Nape Nnauye mara baada ya zoezi la kuvunja kufuli ya lango la
ghala hilo kukamilika. Waziri Nape kwa kushirikiana na viongozi wa
taasisi zinazosimamia maslahi ya kazi za ubunifu wamefanya operesheni
iliyofanikisha kukamtwa kwa shehema kubwa ya kazi haramu za filamu na
muziki kwenye ghala la bwana Ulaya liliofichwa chini ya hoteli ya
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akimfafanulia sheria mbalimbali ambazo mfanyabishara wa kazi za filamu na muziki anastahiki kuzifuata kabla ya kuanza kufanya biashara hiyo. Anaemsikiliaza
Mheshimiwa Nape ni mmiliki wa ghala ambalo shehena kubwa ya kazi haramu
za filamu na muziki zimekamatwa wakati wa operesheni iliyofanyika leo
eneo la Kariakoo jijini Dar-es-Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akikagua rundo la filamu zilizokamatwa kwenye opersheni ya kutokomeza kazi haramu za filamu na muziki nchini. Kwenye operesheni hiyo shehena kubwa ya kazi za
filamu na muziki imekamatwa kwenye ghala lililofichwa chini ya hoteli
ya Butterfly iliyoko mtaa wa Muhonda, Kariakoo jijini Dar-es-salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akisikiliza maelezo kutoka kwa kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Filamu wa Bodi ya Filamu Tanzania Wilhad Tairo wakati wa operesheni ya kutokomeza kazi haramu za filamu na muziki nchini. Operesheni hiyo imefanikisha kukamatwa kwa shehena kubwa iliyokuwa imehifadhiwa kwenye ghala lililofichwa chini ya
hoteli ya butterfly iliyoko mtaa wa Muhonda, Kariakoo.
Pichani ni jengo la hoteli ya butterfly iliyopo mtaa wa Muhonda, Kariakoo
ambalo ghala lenye shehena kubwa ya kazi za haramu za filamu na muziki
0 Comments