Na,Twaha Twaibu
WIZARA ya Maliasili na Utalii imewaasa maofisa vijana
wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) waliohitimu mafunzo yanayowaandaa
kuingia kwenye mfumo wa Jeshi Usu, wasijihusishe na biashara haramu ya wanyamapori na mazao ya
misitu.
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ni
mamlaka iliyoanzishwa kwa Amri ya Serikali na kutangazwa kwenye gazeti la
Serikali Na.135 la tarehe 9 Mei,
2014. Uanzishwaji wa Mamlaka hii ni utekelezaji wa kifungu cha 8 cha Sheria ya kuhifadhi Wanyamapori
Na. 5 ya mwaka 2009.
Mamlaka ya
Wanyamapori imeanza kazi rasmi tarehe 1/Julai/2016. Makao makuu yake kwa sasa
yapo Morogoro katika jengo la Taasisi ya utafiti wa mazao ya misitu (TAFORI).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence S. Milanzi amewataka wahitimu wa mafunzo hayo wasijichukulie sheria mikononi kuwaadhibu watuwanaobainika kuingia ndani ya Mapori ya Akiba, bali wawakamate na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ili sheria ichukue mkondo wake.
alitoa nasaha hizo wakati akifunga mafunzo ya wiki sita ya kuwaandaa watumishi wa wizara hiyo kuingia kwenye mfumo wa kijeshi (Jeshi Usu) katika hafla iliyofanyika tarehe 11/3/2017 kwenye Kituo cha Mafunzo kilichopo wilayani Mlele Mkoani Katavi.
Mafunzo hayo yalianza Januari 30, mwaka huu 2017 kwa maofisa 100 kati yao,
99 wakiwa ni kutoka TAWA na mwingine ni ofisa kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa).Waliohitimu na kuwa tayari kwa majukumu walikuwa 99.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja
Jenerali Gaudence S.
Milanzi akiongea na wahitimu
Milanzi akiongea na wahitimu
Katibu Mkuu
aliwaeleza wahitimu kuwa, ‘ Mimi binafsi natambua kuwa mafunzo haya hayakuwa
rahisi kwenu haswa ukizingatia wengi wenu kama siyo wote, hii ndiyo mara yenu
ya kwanza kupata mafunzo kama haya,lakini kwa dhamira nzuri na yenye mtazamo
chanya mliyokuwa nayo imepelekea wote kumaliza salama. Ni matumaini yangu kuwa
mafunzo haya yatasaidia kuimarisha nidhamu kwenye maeneo yetu ya kazi katika kipindi hiki tunachojianda
kuingia katika mfumo wa kiutendaji wa jeshi usu’’ Nanukuu.
Katibu Mkuu
aliendelea kuwaeleza kwamba, lengo kubwa la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa
kuongoza watumishi walio chini yao ambao wengi ni askari.wakati wahitimu hawa
wengi wao hawajapata mafunzo ya kijeshi tangu wamalize elimu yao ya chuo kikuu.
Katibu Mkuu alisema ,majukumu waliyopewa ni makubwa ambayo lengo lake ni kuwaanda
kuwa wahifadhi wakuu na baadaye. Hivyo ni vyema wakatambua kuwa baada ya
mafunzo haya wanajukumu yanawasubiri mbele yao.
Katibu Mkuu
alisisitiza kwenye hotuba yake kwa
kusema kwamba, Wizara ya Malaisili na Utalii itaendelea na hatua za kuanzisha
mfumo wa Jeshi Usu katika sekta za wanyamapori na Misitu. Hivyo, mpanmgo wa
kutoa mafunzo haya ni endelevu na yatatolewa kwa watumishi wote wanaohusika na
ulinzi wa raslimali za maliasili katika sekta za wanyamapori na misitu. Lengi
ni kudumisha nidhamu na kuongeza ufanisi ili wahifadhi wote waweze kuongea
lugha moja ya uhifadhi.
Akiitimisha hotuba
yake alizungumzia suala la ujangili kwa kusema, Wizara inaamini kwamba
changamomoto za ujangili na uvunaji haramu wa misitu na matatizo mbalimbali
yanayohikabili uhifadhi nchini hayawezi kutatuliwa kwa mfumo wa utendaji kazi
wa kiraia. Hivyo, Wizara inakamilisha taratibu za kubadili mfumo wa utendaji
kazi kutoka wa kiraia kwenda jeshi usu.Mabadiliko haya ya kimfumo ni matakwa ya
Sheria ya Uhifadhi Wanyamapori Na.5 ya mwaka 2009 ambayo imeanisha kwamba
kutaundwa kikosi cha jeshi usu (Wildlife
Protection Unit), ili kuhakikisha ulinzi kamili wa rasilimali katika maeneo
yaliyohifadhiwa
Katika Maadhimisho
hayo pia kulikuwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA, ambaye liwakilishwa na Naibu Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya TAWA Inspekta
Jenerali Abdulrahman Kaniki, kwa kusema,
Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori inafuatilia kwa karibu matayarisho
yanayofanywa ya kuandaa watumishi kuingia kwenye mfumo wa Jeshi usu ili
kuboresha ulinzi wa raslimali za maliasili kwa ujumla.
Inspekta Jenerali
Kaniki, alimalizia hotuba yake kwa kuwajulisha wahitimu kuwa, Bodi ya TAWA inao
wajumbe waliobobea kwenye masuala ya Ulinzi na usalama wa nchi. Watatumia utaalamu
wao kuishauri vizuri mamlaka na Wizara kwa ujumla ili kuhakikisha kwamba mfumo
wa jeshi usu unaanzishwa rasmi ili kuongeza ufanisi katika ulinzi wa raslimali
za maliasili kwa faida ya vizazi vyote.
![]() |
|
Inspekta Jenerali Abdulrahman Kaniki (wa kwanza kushoto mwenye
koti akiangalia gwaride la wahitimu
|
Maafisa wanayamapori kutoka TAWA wakiwa taryari kutoa
heshima kwa mgeni rasmi
Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa TAWA Bw. Martin T.Loibooki, alianza hotuba yake kwa kumshukuru Katibu
Mkuu kukubali kuja kufunga mafunzo hayo ya Maafisa wanyampori daraja la 11
kutoka TAWA na TANAPA.
Bw.loibooki
alielezea kidogo Mamlaka anayoisimamia kwa kuanza kusema, Mamlaka ilianzishwa
na Serikali kama chombo cha utekelezaji wa majukumu ya Serikali kwa niaba ya
Serikali chini ya uangalizi wa Serikali na
kuwa na mfumo unaonesha utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi zaidi. Kama
ilivyo kwa Mamlaka Serikali nyingine nchini, lengo la kuanzishwa TAWA ni
kutekeleza majukumu ya Idara ya Wanyamapori hasa ya Usimamizi wa Wanyamapori
nchini. Majukumu ya TAWA ni kusimamia
shughuli za utawala, ulinzi, usimamizi wa raslimali ya Wanyamapori katika
maeneo yote nje ya Hifdahi za Taifa na Hifadhi ya Ngorongoro.
BW.MARTIN T. LOIBOOKI (KAIMU MKURUGENZI MKUU –TAWA)
Baada ya maelezo
hayo mafupi, Bw.Loibooki alimueleza mgeni rasmi kuwa, kozi ya kwanza ya mafunzo
haya ilifanyika mwezi Oktoba, 2016 ambayo ilihusisha Maafisa wanyamapori daraja
la pili 40. Na hii ni ya pili ambayo tunaishuhudia leo imejumuisha watumishi
99. Hivyo jumla Mamlaka inakuwa na jumla ya watumishi 139 amabo wamepata
mafunzo katika kituo cha Mlele.
Bw.Loibooki alisema
kwa kukamilika kwa kozi hii ni faraja kub wa sana kwa Mamalaka kwani kundi hili ndilo
lilikuwa na changamoto kubwa za kiutendaji kwa kutokuwa na msingi wa mafunzo ya
kijeshi.
Aliendelea kumueleza
mgeni rasmi kuwa, kwa kuanzia kozi mbili zilizofanyika katika kituo cha Mlele
zilihusisha Maafisa wanyamapori kutoka TAWA ambao waliajiriwa kutoka vyuo vikuu
lakini hawakupata mafunzo ya awali ya kijeshi. Maafisa hawa ndiyo wasimamizi wa
askari katika kazi za kila siku pamoja na doria.Hivyo,kulikuwa na upungufu
mkubwa kiutendaji kwa wahifadhi ambao hawakupata mafuzo ya kijeshi kuwasimamia
waliopata mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mkuu
alimueleza mgeni rasmi kuwa mwezi Februari 2017.Mamlaka ilikamilisha draft ya
Sheria yake (The Tanzania Wildlife Management Authority Act of 2017) Sheria
itakapopitishwa itaongeza nguvu ya utekelezaji wa mfumo wa Jeshi usu. Aidha,
Taasisis za wanyamapori zimeandaa draft ya kanuni za jeshi usu (The wildlife
protection regulations) ambazo zipo katika hatua ya kupitiwa na Menejement ya
Wizara kabla ya kuidhinishwa na Mheshimiwa Waziri wa Malaisili na Utalii.
Bw. Loibooki
alimueleza mgeni rasmi kuwa TAWA imeunda kikundi kazi cha kuanda TAWA General Orders ambao utakuwa
muongozo wa utekelezaji wa kazi za kila siku.
Alimaliza hotuba
yake kwa kusema kwamba mamlaka ianjipanga na inachukulia kwa makini wa hali ya
juu maandalizi ya kuingia mfumo wa jeshi usu.
Bw.Loibooki alihitimisha
hotuba yake kwa kusema kwamba, katika mwaka wa fedha 2017/18 ,mamlaka imetenga
fedha kwa ajili ya kuendelea kutoa mafunzo ya utayari wa kupokea mabadiliko
kuelekea katika mfumo wa jeshi usu.Watumishi wote watapata mafunzo hayo kufuata
ratiba itakayowekwa na mamlaka.Ratiba ya mafunzo itawekwa bayana ili kuwatoa
hofu watumishi na kuwapa nafasi ya kufanya maandalizi mapema. Mwezi Mei 2017
,mamlaka italeta watumishi wengine kwenye mafunzo.Kozi hii itakuwa ni maalum
kwa wakuu wa vituo na baadhi ya maafisa wa makao makuu.
Mhitimu toka TAWA akitoa heshima kwa Katibu Mkuu
Kaimu mkurugezi mkuu wa TAWA Bw,Martin Loibooki anena
neno na Mkuu wa chuo cha Taaluma ya Wanyamapori pasiansi Bi.lowael Damalu







0 Comments