Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea Bandari ya
Zanzibar, ikiwa na lengo la kukagua
mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa Dawa za Kulevya huku akiliagiza Jeshi la
Polisi Zanzibar kushirikiana na Uongozi wa Bandari, kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili
kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo humaliza nguvu kazi ya Taifa. Wakwanza
kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar, Mohamed Ahmada Salum na anayefuatia ni Mkurugenzi Mkuu
Bandari ya Zanzibar, Kapteni Mstaafu Abdula Juma.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni, akitembea kuelekea sehemu inayokaguliwa mizigo wakati wa ziara ya kutembelea Bandari ya
Zanzibar, ikiwa na lengo la kukagua mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa Dawa za
Kulevya, huku akiliagiza Jeshi la Polisi Zanzibar, kushirikiana na Uongozi wa
Bandari kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa dawa
hizo ambazo humaliza nguvu kazi ya Taifa.Wakwanza kulia ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed Ahmada Salum na
anayefuatia ni Mkurugenzi Mkuu Bandari ya Zanzibar, Kapteni Mstaafu Abdula
Juma.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni, akikagua jinsi ukaguzi wa mizigo unavyofanyika kupitia
komputa wakati wa ziara ya kutembelea Bandari ya Zanzibar ikiwa na lengo la
kukagua mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa Dawa za Kulevya, huku akiliagiza
Jeshi la Polisi Zanzibar kushirikiana na Uongozi wa Bandari kuhakikisha ukaguzi
wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo humaliza nguvu
kazi ya Taifa. Kulia ni Afisa wa Bandari anayeshughulika na ukaguzi, Adam
Masoud.
Mfanyakazi wa kitengo cha mizigo Bandari ya
Zanzibar, Saleh Masoud akikagua moja ya mzigo wa abiria wanaoingia kupitia
bandari hiyo ambapo Naibu Waziri
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,ameliagiza Jeshi la
Polisi Zanzibar kushirikiana na Uongozi wa Bandari hiyo kuhakikisha ukaguzi wa
mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa Dawa za Kulevya ambazo zimekuwa
zikiharibu nguvu kazi ya Taifa.
Mkurugenzi Mkuu Bandari ya Zanzibar, Kapteni
Mstaafu Abdula Juma (wapili kushoto), akimsikiliza Naibu Waziri Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa ziara ya kutembelea bandari hiyo ikiwa na lengo la kukagua mifumo ya udhibiti
wa uingizwaji wa Dawa za Kulevya huku akiliagiza Jeshi la Polisi kushirikiana na Uongozi wa Bandari kuhakikisha
ukaguzi wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo
humaliza nguvu kazi ya Taifa.Wakwanza kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mohamed Ahmada Salum
na wakwanza kulia ni Kamishna wa
Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu.
Kifaa cha kubebea
kontena kikiwa kimebeba kontena tayari kupelekwa kwenye mashine maalumu ya
ukaguzi ambayo hutumia mionzi kukagua mzigo uliopo ndani, ambapo Naibu Waziri
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameliagiza Jeshi la Polisi kushirikiana na
Uongozi wa Bandari ya Zanzibar kukagua
mizigo yote inayoingia ili kudhibiti uingiaji wa Dawa za Kulevya Visiwani
Zanzibar.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI






0 Comments