Waziri wa Habari, Utamaduni, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Jijini Dar es Salaam. Wapili
kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya kiapo Waziri Mpya wa Habari, Utamaduni,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe katika hafla iliyofanyika
leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba John
Aidan Mwaluko Kabudi akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni
Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi.
Katibu Mkuu, Ikulu Alpayo Kidata akila kiapo
mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo
Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi
John Kijazi.Kabla ya uteuzi huo Kidata alikuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA).
Balozi Dkt. Abdallah Saleh Possi akila kiapo
mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo
Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi
John Kijazi. Balozi Dkt. Possi ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini
Ujerumani.
Balozi Job Massima akila kiapo mbele ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani) leo
Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John
Kijazi. Balozi Massima ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Israel.
Balozi Sylivester Mabumba akila kiapo mbele ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Jijini Dar
es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi. Balozi
Mabumba ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania katika Visiwa vya Comoro.
Kamishna wa Tume ya Mahakama Mhe. Jaji Stella
Esther Mugasha akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli (hayupo pichani) leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi.
Baadhi ya Makatibu Wakuu na Manaibu Waziri
wakifuatilia hafla ya kuapishwa kwa Mawaziri wawili, Katibu Mkuu Ikulu,
Mabalozi wanne na Kamishna wa Tume ya Mahakama, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha
ya pamoja na viongozi walioapishwa katika hafla liyofanyika leo Ikulu Jijini
Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili Jaji
Mstaafu Harold Reginald Nsekela, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John
Kijazi, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan,Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa
Ibrahim Juma, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju.
PICHA
ZOTE NA MAELEZO.
......
Na. Immaculate Makilika-
MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaasa waandishi wa habari nchini kuandika
habari zinazohamasisha maendeleo ya nchi badala ya kuandika habari ambazo
hazina manufaa kwa taifa.
Akizungumza wakati ya hafla ya
kuwaapisha mawaziri, mabalozi pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu jijini
Dar es Salaam leo, Rais Magufuli alisema kuwa waandishi wa habari wanatakiwa
kuwa wazalendo kwa kuandika habari za kuhamasisha wananchi kushiriki katika
shughuli za maendeleo pamoja na kuunga mkono jitihada mbalimbali za Serikali.
“Nchi yetu ina sifa nzuri nje,
Rais wa Benki ya Dunia alipotembelea katika nchi yetu hivi karibuni
alitupatia jumla ya shilingi trilioni 1.74 na benki hiyo ipo mbioni
kutupatia fedha nyingine shilingi trilioni 2.8, lakini vyombo vyetu vya habari
haviandiki kwa mapani juu ya taarifa ” alisema Rais Magufuli.
Alibainisha kuwa fedha hizo
zitatumika katika miradi ya Ujenzi wa barabara za juu eneo la Ubungo, maboresho
ya miji, pamoja na Vyuo Vikuu vya Sokoine na Mandela na kuleta
maendeleo ya nchi yetu lakini taarifa zake hazikupewa uzito unaostahiki katika
vyombo vya habari.
Rais Magufuli aliwataka
wamiliki wa vyombo vya habari pamoja na waandishi wa habari kufuata uweledi wa
taaluma ya habari pamoja na kuweka mbele maslahi ya taifa badala ya maslahi ya
mtu mmoja mmoja.
Aidha, Rais Magufuli
amewapongeza viongozi aliowaapisha na kuwataka kufanyakazi kwa bidii na
juhudi ili kutimiza azma ya serikali ya kuwa nchi ya uchumi wa kati kwa
kutekeleza agenda ya viwanda.
Viongozi walioapishwa ni Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, Waziri wa
Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,
Alfayo Kidata.
Wengine ni Balozi wa Tanzania
nchini Ujerumani Dkt. Abdallah Possi, Balozi wa Tanzania nchini Israel Job
Masima, Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Sylvester Mabumba pamoja na
Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Stellah Mugasha.













0 Comments