Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC, Eng. Kapuulya Musomba .
Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC) limesema mpaka kufikia mwaka 2020 litawawezesha watanzania kutumia
gesi majumbani mwao hivyo kupelekea upungufu wa uharibifu wa mazingira nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa TPDC Eng. Kapuulya Musomba
amesema muda mrefu kumekuwa na uharibifu wa mazingira hivyo kupatikana kwa
nishati ya mafuta na gesi kutaiwezesha Tanzania kuwa mahali salama kimazingira
ikiwa ni pamoja na ukuaji wa sekta ya uchumi.
Alisema katika robo ya pili ya mwaka 2017 shirika
limekamilisha usambazaji wa mabomba ya gesi kwa matumizi ya majumbani jijini
Dar es Salaam na zaidi ya viwanda 300 vimeunganishwa na nishati ya gesi hapa
nchini hivyo kupelekea upatikanaji wa umeme wa uhakika.
Kuhusu upangaji wa Bei kwa matumizi ya gesi
itakayosambazwa majumbani Eng. Musomba amesema Taasisi yake itashirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), kuhakikisha nishati hiyo inapatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu.
Hivi
sasa zaidi ya asilimia 50 ya umeme uliopo katika Gridi ya Taifa unatokana na
gesi asilia hivyo mipango ya Serikali ni kulifanya Shirika hilo kuchangia zaidi
mapato Serikalini yanayotokana na rasilimali hiyo.Alisema Eng. Musomba
Alisema
TPDC imejipanga kuwekeza kwenye shughuli za utafutaji, uzalishaji, usafirishaji
na usambazaji wa gesi ili Taifa linufaike na rasilimali hiyo.
Akitolea mfano mradi mkubwa wa kusindika gesi
asilia (Liqufied Natural Gas-LNG), Eng. Musomba alifafanua kwamba itachukua
takribani miaka 8 hadi 10 kabla ya mzigo wa kwanza wa LNG kusafirishwa kwenda
katika soko la dunia kwa mauzo.
Alisema kukamilika kwa mradi wa (Liqufied Naturla Gas- LNG)utakuwa
ni fursa kwa watanzania kupata ajira katika mradi huo ikiwa ni pamoja na kuchangia
pato la mwananchi,wawekezaji na Taifa kwa ujumla.
Alisema uwekezaji katika sekta ya mafuta na gesi
ni wa gharama kubwa na hata mafaniko kwa maana ya mapato makubwa kwa Serikali
huchukua muda mrefu kuonekana hivyo amewataka wananchi kuwa wazalendo kwa
kuilinda miundombinu inayopita maeneo yao.
TPDC inaendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali
ikiwa na lengo la kuongeza uelewa zaidi katika sekta hiyo ya gesi na mafuta.

0 Comments