Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa Zanzibar , Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na vyombo vya habari katika eneo
la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa wa Mjini Magharibi ambalo matendo ya uhalifu
ikiwepo utumiaji wa dawa za kulevya na uporaji
hufanyika hapo ambapo ameuagiza uongozi wa Jeshi la Polisi kushirikiana
na wananchi kuhakikisha wahalifu hao wanakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya
sheria
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia
jeraha la mmoja wa wananchi wa eneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa wa
Mjini Magharibi, ambaye wiki chache zilizopita alijeruhiwa na mapanga na watu
wanaofanya matendo ya uhalifu katika eneo hilo
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mjini Magharibi, ASP Suleiman
Khamis Juma, akizungumza na vyombo vya habari juu ya hatua zilizochukuliwa na
Jeshi la Polisi kudhibiti matukio ya uhalifu katika eneo la Mwanyanya
Mikoroshini lililopo mkoa huo, wakati wa ziara ya Katibu wa Kamati Maalum ya
NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo
pichani) kutembelea maeneo sugu ya uhalifu.
Katibu wa
Kamati Maalum ya NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza
na Mkuu wa Upelelezi
Mkoa wa Mjini
Magharibi, ASP Suleiman Khamis Juma (kushoto), baada ya kutembelea eneo la
Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa huo ambalo matendo ya uhalifu ikiwepo utumiaji wa
dawa za kulevya na uporaji hufanyika ambapo Katibu huyo wa NEC ameuagiza uongozi wa Jeshi la Polisi kushirikiana
na wananchi kuhakikisha wahalifu hao wanakamatwa.
Mkuu wa Polisi Wilaya
ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ally Kitole, akimueleza Katibu wa Kamati Maalum ya NEC
Idara ya Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa Zanzibar, Mhandisi Hamad
Masauni baadhi ya hatua walizochukua katika kupambana na uhalifu unaoatokea
eneo la Mwanyanya Mikoroshini.
Picha na Abubakari Akida





0 Comments