Makomandoo wa
Jeshi la wananchi wa Tanzania wakionesha umahiri wao wa kuvuta gari lenye tani 7
ikiwa ni moja ya mbinu ya medani katika uwanja wa mapambano.
Askari wa
Kikosi cha Farasi wakionesha umahiri wao katika kutumia farasi kupambana na
uhalifu.
Wanafunzi wa halaiki
wakipita kwa ukakamavu mbele ya Jukwaa Kuu.
Vikosi
vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya maadhimisho ya Maadhimisho
ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika
terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.
Askari wa Pikikipi
maalum wakionesha namna pikipiki hizo zitakavyopamba maonesho hayo.
Mhagama akikagua maandalizi ya kuadhimisha Sherehe za Miaka 53
ya Muungano katika viwanja vya Jamhuri leo Mjini Dodoma.
....
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO - DODOMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Uratibu, Ajira na Wenye ulemavu, Jenista Mhagama amewaasa Watanzania kuwa
wazalendo pamoja na kudumisha amani na utulivu uliopo nchini.
Akizungumza, leo mjini Dodoma wakati akifuatatilia
maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano yatakayofanyika Aprili 26
mwaka huu katika Uwanja wa Jamhuri uliopo mjini Dodoma.
“Tunapoadhimisha miaka 53 ya Muungano ninawaomba
watanzania kuwa wazalendo pamoja na kulinda amani ya nchi” alisema Waziri
Mhagama
Pia, Waziri Mhagama aliwaomba watanzania hasa wakazi
wa Dodoma kuhudhuria kwa wingi katika Maadhimisho hayo yatakayofanyika jumatano
wiki hii.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana
alisema kuwa mkoa wake umejipanga vizuri katika kufanikisha maadhimisho hayo,
ambapo pia alivishukuru vyombo vya habari kwa kuhamasisha wananchi juu ya
maadhimisho hayo.
“Wananchi wamehamasika kushiriki katika maadhimisho
haya ya miaka 53 ya Muungano, ninawashukuru kwa kazi kubwa mliyoifanya na
tunaamini mtaendelea kuhamasisha wananchi kushiriki katika maadhimisho hayo”
alisema Rugimbana
Maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano
yamehudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Christina Mndeme, pamoja na
viongozi mbalimbali wa Serikali.
Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo,
ambapo pia yatahudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein na viongozi mbalimbali wa dini na Serikali.
Maadhimisho hayo ya miaka 53 ya Muungano yanatarajiwa
kupambwa namaonesho kutoka kutoka vikosi
mbalimbali vya ulinzi na usalama, burudani za vikundi vya ngoma pamoja na maonesho ya halaiki.







0 Comments