14
APRIL 2017
Chama cha Mapinduzi CCM kimetoa salamu za pole
kwa Mwenyekiti wa Chama hicho Rais Dkt. John Pombe Magufuli kufuatia kuuwawa
kwa askari polisi nane kwa kushambuliwa
na watu wenye silaha katika eneo la Jaribu Mpakani ,Wilaya ya kibiti mkoani Pwani.
Salamu hizo zimewasilishwa kwa Rais
Magufuli na Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Ndg. Humphrey Polepole Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Akiwa ameambatana na Naibu Katibu Kuu CCM
Tanzania Bara Rodrick Mpogolo na Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Bi Amina
Makilagi, Ndugu Polepole amesema kwa kuwa Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi CCM ndio Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri
Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, hivyo ndio maana CCM imeshtushwa na
tukio hilo na kutoa pole hizo kutokana na kuuwawa kwa askari hao ambao wamekuwa
na jukumu kubwa la kulinda usalama wa wananchi na mali zao .
Amesema askari hao wamekuwa wakifanya kazi
katika mazingira magumu wakati wote kuhakikisha watanzania wanakuwa salama
pamoja na mali zao hivyo tukio la kuuwawa kwao ni jambo la kusikitisha sana.
Pia Polepole amesema wamekutana na
Mheshimiwa Rais kumueleza mchakato wa Uchaguzi wa ndani wa CCM ambao unaendelea
nchini kote kuanzia ngazi ya mashina hadi taifa.
Aidha amesema CCM inampongeza Rais
Dkt.Magufuli kwa kitendo cha kizalendo cha serikali ya awamu ya tano kutumia fedha zake za ndani katika ujenzi wa
Reli itakayokuwa na kiwango cha kimataifa yenye urefu wa kilomita 300 kutoka
Dar es salaam hadi Morogoro.
Amesema ujenzi wa reli hiyo yenye kiwango
cha kimataifa itakayotumia treni ya umeme inadhihirisha jinsi CCm
inavyojishughulisha na shida za watu.


0 Comments