Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Juma Masenza,
akifanya mazungumzo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Ndugu Andrew W. Massawe,
wakati alipomtembelea Mkuu wa Mkoa makao makuu ya mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina
Juma Masenza akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
NIDA walipotembelea ofisi yake. Katikati ni Mkuu wa Mkuu wa Mkoa, akifuatiwa na
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA katikati kulia. Na wa kwanza kulia ni Ndugu
Alphonce Malibiche Kaimu Mkurugenzi Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa NIDA na
wa kwanza kulia ni Bi. Rose Mdami Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na
Hifadhi Hati.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa NIDA ndugu, Andrew W. Massawe
akifafanua jambo wa Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Juma Abdallah
wakati wa alipotembelea ofisi ya Mkuu huyo wa Wilaya Kilolo – Iringa
Katika majadiliano ni
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilolo Mhe. Mwl. Valence Kihwaga na ujumbe wake
wakizungumza na ujumbe wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA kwenye makao makuu ya
Halmashauri hiyo – Kilolo
Kaimu Mkurugenzi Mkuu
akizungumza na watumishi wa NIDA wanaofanya kazi katika Ofisi ya Wilaya ya
Kilolo - Iringa
Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Mhe. Amina Juma Masenza; amemhakikishia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Ndugu
Andrew W. Massawe mkoa wake kumaliza ndani ya siku 60 zoezi la kuwasajili
wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea wanaishi mkoani humo.
Ahadi hiyo ameitoa leo
alipofanya mazungumzo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, wakati alipomtembelea
ofisini kwake makao makuu ya mkoa huo yaliyopo Iringa; ikiwa imesalia moja
kabla ya kufanya uzinduzi rasmi wa kuanza kuwasajili wananchi katika Wilaya
zote za Mkoa wa Iringa.
Akifafanua kwanini Mkoa
wa Iringa umeamua kuwasajiliwa wananchi wake wote kupata Vitambulisho vya
Taifa; Mkuu huyo wa Mkoa amesema mafanikio makubwa ya zoezi la kuwasajili
watumishi wa Umma ni moja ya kichocheo kikubwa cha mkoa wako kuona umuhimu kuwa
kuwatambua wananchi wake wote ili kuwa na idadi sahihi wa wakati wa mkao wa
Iringa; zoezi linaloenda sambamba na kuwasajili wageni wanaoishi kihalali
nchini.
“ kama Mkuu wa Mkoa
nimejifunza na kutambua umuhimu mkubwa sana wa Vitambulisho vya Taifa kwa mtu
binafsi lakini pia kwa maendeleo ya mkoa, hivyo sioni sababu kwanini tusitumie
fursa iliyopo kuwasajili wananchi wetu wakati uwezo wa kufanya hivyo tunao”
alisitiza.
Kabla ya kutembelea
ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA alifanya ziara
kutembelea Wilaya ya Kilolo na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.
Asia Juma Abdallah ambaye alimhakikishia mkurugenzi huyo ushirikiano katika
kufanikisha zoezi hilo.
Naye Mwenyekiti ya
Halmashauri ya Kilolo Mhe. Mwl. Valence Kihwaga amesema Waheshimiwa Madiwani
wako tayari kushiriki katika zoezi hilo na wamejipanga katika kuhakikisha
wananchi wao wanapata huduma hiyo.
Mkoa wa Iringa umepanga kufanya rasmi
uzinduzi wa kuanza kwa zoezi la kuwasajili Vitambulisho vya Taifa, Wananchi wa
mkoa wa Iringa pamoja na kuanza utoaji Vitambusho vya Taifa kwa wananchi katika
Wilaya ya Mufindi.
Katibu Tawala katika Mkoa huo amethibitisha tukio hilo na kuanisha
mipango ambayo itatumika katika kuhakikisha wananchi wote wanasajiliwa katika
kipindi cha siku 60 zilizobainishwa na Uongozi wa Mkoa.





0 Comments