Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala
Bora Mhe. Angella Kairuki akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha
kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
Na
Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma
Serikali
imewasahuri wananchi wote wanaofaidika na Mpango wa kunusuru Kaya Maskini
(TASAF) nchini kuzitumia vizuri ruzuku wanazozipata kwa kuendelea
kujishughulisha na shughuli za kiuchumi katika maeneo yao.
Akijibu
swali la Mbunge wa Mtabwe Mhe. Khalifa Mohamed Issa lililouliza Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF) upo katika Awamu ya Tatu ya Utekelezaji wa Mpango wa
kunusuru Kaya Maskini nini kimefanyika ili ruzuku ziweze kumudu mahitaji ya
chakula, Elimu, Afya na lishe Bora kwa watoto.
Waziri
wa Nchi ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki amesema
kuwa Serikali inaendelea kutoa ruzuku wa Kaya Maskini ila inasahuri pia wananchi
waendelee kujishughulisha na kazi nyingine za kuongeza kipato na isitegemee
ruzuku pekee.
“Niwaombe
wananchi wanaopata ruzuku kutoka mpango wa TASAF wajishughulishe pia na shughuli
nyingine za kiuchumi na kutotegemea ruzuku pekee” Alisistiza Mhe. Angella.
Ameongeza
kuwa ruzuku zinazotolewa ni kichocheo cha kuifanya kaya iweze kujikimu hasa
katika kupata mahitaji muhimu huku ikiendelea kujiimarisha kiuchumi kwa kuweka
akiba na kutekeleza miradi ya ujasiriamali ili iweze kusimama yenyewe na
kujitegemea baada ya kutoka katika umaskini uliokithiri.
Mhe.
Angella Kairuki ameeleza kuwa vigezo vya kupata kaya maskini ni wa uwazi na huanishwa
na Jamii katika mkutano wa hadhara unaoendeshwa na wawezeshaji kutoka
Halmashauri za Wilaya na kusimamiwa na Viongozi wa Vijiji, Mitaa na Shehia.
Aidha
uzoefu uliopatikana umeonesha kwamba kwa kiwango cha ruzuku kinachotolewa kwa
wananchi wanaofaidika na Mpango huo kimewawezesha kuboresha maisha yao kwa
kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi zikiwemo ufugaji,ujasiriamali na ujenzi wa nyumba bora, hivyo viwango hivyo sio
vidogo kama wengi wanavyodhani.

0 Comments