Nyumba mbalimbali zikionekana kubomoka na kuezuliwa mapaa na mvua iliyoambatana na upepo ambayo imenyesha huko Chalinze Mzee ,jimbo la Chalinze mkoani Pwani. Kufuatia maafa hayo, mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete amewatembelea waathirika waliokumbwa na adha hiyo.
(Picha na Mwamvua Mwinyi)
.........
Na Mwamvua
Mwinyi
MVUA
inayoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali mkoani Pwani hususan,
jimbo la Chalinze imeleta madhara huko eneo la Chalinze Mzee ambapo
kaya zaidi ya 20 zimekosa makazi ya kuishi.
Aidha nyumba tisa zimesombwa na maji na
nyingine kubomoka hali inayosababisha wakazi wa nyumba hizo kuishi kwa
kusaidiwa na ndugu na majamaa.
Kutokana na hali hiyo, mbunge wa Jimbo la Chalinze
,Ridhiwani Kikwete,ametembelea eneo la Chalinze Mzee lilokumbwa na mafuriko
kutokana na mvua hizo.
Ridhiwani alitoa pole kwa waathirika
waliokumbwa na maafa hayo .
Alitaja maeneo yaliyokumbwa na mafuriko
ni Chalinze Mzee,Bwawa la umwangiliaji la Msoga ambalo limetoboka na shule ya
Sekondari ya Imperial.
Aidha,Ridhiwani alieleza kuwa madhara makubwa
yaliyotokana na mafuriko hayo ni kuharibika kwa mashamba,nyumba za wananchi kuharibika
na wananchi kukosa pakuishi.
Mbunge huyo aliongeza kwamba kwasasa wananchi
hao wanahitaji msaada hivyo aliwaomba wadau wa maendeleo ya jamii kuwasaidia
kwa hali na mali.
"Ni maafa makubwa inabidi yatuguse
wote niwaombe wadau wengine washirikiane
na serikali na mi mbunge kuwawezesha yale yaliyokwenye uwezo wetu watu hawa
"alisema Ridhiwani.
Kwa upande wao baadhi ya wakazi waliokumbwa na
kadhia hiyo walisema mvua iliyoambatana na upepo mkali ,imeezua mapaa ya nyumba
na nyingine kubomoka na kusababisha familia za nyumba hizo kuhaha kukosa pakuishi.
No comments:
Post a Comment