Toka atue Manchester United kwa rekodi ya usajili ya dunia, Paul
Pogba amekuwa akiongelewa sana haswa kuhusiana na kiasi cha pesa ambacho
Manchester United wamemnunua na kiwango anachoonesha.
Hata kabla hajaanza kucheza wengi walisema pesa za kumnunulia Pogba
ni bora kununua mshambuliaji ambaye kila wiki anafunga, tabu zaidi
ilianza baada ya Pogba kuingia uwanjani japokuwa haoneshi kiwango kibovu
sana lakink ameshindwa kufikia kile kiwango walichotaraji mashabiki.
Sio tu mashabiki wa soka bali na wachambuzi mbali mbali wamekuwa
wakimuongelea Pogba,na wote kelele zimekuwa zile zile kuhusu pesa
aliyosajiliwa na kiwango anachoonesha, lakini mara zote kocha wake Jose
Mourinho amekuwa ndio mtetezi pekee wa kiungo huyo wa Kifaransa.
Na sasa kwa mara ya kwanza Pogba amesimama mbele ya waandishi wa
habari na kuongea kuhusu dau lake na kuwajibu wale wote wanaozungumzia
sana kuhusu dau lake, kwanza Pogba ameshangazwa na jinsi watu
walivyoacha mambo mengi na kumuangalia yeye tu na kuhoji kuhusu ufungaji
kanakwamba yeye ni mshambuliaji.
“Watu wananiangalia mimi tu na kuanza kunihukumu kwanini sifungi na
mambo mambo mengine, mimi ni kiungo lakini kama ningekuwa ninafunga
wasingeongea lolote, ona wengine wanazungumzia kuhusu dau langu la
usajili lakini usajili ni jambo lingine na uwanjani ni lingine” alisema
Pogba.
Pogba alimalizia kwa kusema kwamba yeye anafanya kazi iliyomleta Old
Trafford na kazi yenyewe ni kucheza kiungo na sio mshambuliaji, ila
akitengeneza nafasi na watu hawafungi hilo sio jukumu lake.


0 Comments