Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli ametoa wito kwa
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kufungua ubalozi wa Israel hapa nchini.
Rais
Magufuli alisema hayo Alhamisi hii alipokutana na balozi wa Israel hapa
nchini, Yahel Vilan Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais alimhakikishia
balozi huyo kuwa Tanzania imedhamiria kuimarisha na kukuza uhusiano na
ushirikiano wake na taifa hilo.
Katika
taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasilino ya Rais, Ikulu, Rais
Magufuli amesema ili kufanikisha dhamira hiyo Tanzania imefungua ubalozi
nchini Israel na amemuomba balozi huyo kupeleka ujumbe kwa Netanyau
kuhusu nchi hiyo kufungua ofisi za ubalozi nchini.
Rais
Magufuli amemuhakikishia kuwa Tanzania imedhamiria kuimarisha na kukuza
zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Israel hususani kwenye masuala ya
uwekezaji, biashara, utalii na uboreshaji wa huduma za jamii.
Aidha
Rais Magufuli alisema ili kufanikisha dhamira hiyo Tanzania imefungua
Ubalozi Isarael na amemuomba Mhe Yahel Vilan kupeleka ujumbe kwa waziri
mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuwa Tanzania itafurahi kuona Israel
inafungua ubalozi wake hapa nchini.


0 Comments