Na Daudi
Manongi-MAELEZO.
Serikali kupitia
Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imelipa madeni ya fedha za likizo kwa
walimu 86,234 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 na 2016/17.
Hayo yamebainishwa na
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Stella Manyanya wakati akijibu
hoja mbalimbali za wabunge Mjini Dodoma.
“Serikali inaendelea
kulipa madeni mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha za likizo kwa
walimu/Watumishi katika sekta ya Elimu”,Aliongeza Mhe.Manyanya.
Amesema kuwa katika
kipidi cha mwaka wa fedha 2015/16 hadi mwezi Juni, 2016 jumla ya shilingi
bilioni 22,629,352,309 zililipwa kwa walimu 63814, na pia katika kipindi cha
mwaka wa fedha 2016/17 hadi kufikia mwezi Machi, 2017 jumla ya shilingi bilioni
10,505,160,275 zimelipwa kwa walimu 22420.
Aidha katika malipo
haya jumla ya shilingi 13,415,410 zimelipwa kwa ajili ya madeni ya fedha za
likizo kwa watumishi wa chuo cha ualimu Korogwe.
Akizungumzia upande
wa upandishaji madaraja Mhe.Manyanya amesema kuwakwa sasa uhakiki wa watumishi
unaendela na ukikamilika watapandisha madaraja kama inavyotakiwa.
Aidha amesisitiza
kuwa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia
imekuwa ikiwapandisha vyeo watumishi
wake wenye sifa kila mwaka ambapo
katika mwaka 2015/16 Wizara iliwapandisha vyeo watumishi 2272 kati yao
watumishi 71 ni wa chuo cha ualimu korogwe.
Uhakiki wa madeni ya
miaka ya nyuma unaendelea kuratibiwa na mamlaka husika na taratibu za malipo
zitakamilishwa kwa wale wanaostahili.

0 Comments