Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Dkt. Harison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Simba ukiongozwa na Rais wake
Bw. Evans Aveva Mjini Dodoma.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harison Mwakyembe
akizungumza na uongozi wa Simba ukiongozwa na Rais wake Bw. Evans Aveva Mjini
Dodoma.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WHUSM Dodoma.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Dkt Harrison Mwakyembe amekutana na na uongozi wa klabu ya Simba ukiongozwa na
Rais wake Bw. Evans Aveva kwenye Ofisi zake Mjini Dodoma.
Uongozi wa Simba umeitikia wito wa Mhe. Mwakyembe
wa kukutana naye na kujadili masuala mbalimbali ya mpira wa Miguu zikiwemo
fursa na changamoto katika mabadiliko na maedneleo ya uendeshaji wa timu.
Aidha Mhe.
Mwakyembe amepokea maoni ya Uongozi wa
samba na kusahauri kuendelea kutoa ushirikiano na wadau wa mpira wa miguu
nchini.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara husika prof Elisante
Ole Gabriel, Mkurugenzi wa Michezo Yusufu Omary, Katibu Mkuu wa BMT Mohamed
Kiganja, na Msajili wa Vilabu na Vyama nchini.


0 Comments