WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO YATOA PONGEZI KWA MHE. PAUL MAKONDA - MTAZAMO MEDIA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Saturday, 8 April 2017

demo-image

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO YATOA PONGEZI KWA MHE. PAUL MAKONDA

Responsive Ads Here



pic%252Bmakonda
Capture
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo yenye dhamana ya kusimamia Maendeleo ya sekta ya filamu nchini, inatoa pongezi kwa Mhe. Paul Makonda; Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-salaam kwa kuunga mkono jitihada za Wizara za kuendesha  operesheni dhidi ya kazi  haramu  za filamu, kazi ziziso na maadili  pamoja nakuwachukulia hatua  wafanyabiashara wanaouza kazi hizo. Dhamira ya Mkuu wa Mkoa inalenga ulinzi wa jamii dhidi ya kazi chafu na pia kutetea maslahi na haki za wadau wa tasnia ya filamu.

Wizara pia inaunga mkono tamko la Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuzipiga marufuku filamu za utupu na kuwachukulia hatua wanaoziuza,sambaza na wanazionesha filamu za aina hiyo kwenye vibanda visivyo rasmi. Hatua hizi za Mkuu wa Mkoa ni utekelezaji wa Sheria mbalimbali za nchi ikiwemo Sheria yenye kusimamia Filamu na ile ya hakimiliki na hakishiriki.

Wizara itashirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na vyombo vya Ulinzi na Usalama katika kuhakikisha dhamira hii njema inatekelezwa na inakuwa endelevu kwa kuhusisha nchi nzima; na inatoa wito kwa Wakuu wa Mikoa yote nchini kuunga mkono jitihada hizi za Serikali katika maeneo yao.

Wizara inapenda kuwahakikishia watanzania kwamba ni haki ya msingi kupata burudani stahiki katika maeneo yao kupitia mifumo mbalimbali ya usambazaji wa kazi za filamu hata hivyo haitawavumilia wale wote wanaoendesha shughuli hizo kinyume cha sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.

 Aidha, inatoa rai kwa wafanya biashara,wadau wa filamu na umma kwa ujumla kuzingatia Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza na Kanuni zake,  Kanuni za Stempu kwa bidhaa za Filamu na Muziki za mwaka 2013 kabla ya kuingiza nchini, kuzalisha, kuonyesha na kuzipeleka kwa walaji kupitia njia yoyote ya kusambaza kazi hizo.


“Filamu ni uchumi Filamu ni ajira, tutumie filamu kuchochea maendeleo endelevu”

Capturemmm

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *