Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewaomba viongozi na wananchi wa Tanzania Bara na Visiwani kushirikiana kwa pamoja kuimarisha na kuulinda Muungano ulioachwa na waasisi wa Taifa wa Shehe Abeid Amani Karume na hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Waziri mkuu aliyasema hayo mara baada ya kushiriki hitma na kuzuru kaburi la Sheikh Karume lililoko Afisi Kuu za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui mjini Unguja wakati wa maadhimisho ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Shehe Abeid Karume sambamba na siku ya mashujaa Zanzibar.
“Ni muhimu kwa wananchi kutenga muda wao na kuwaombea viongozi wetu waliotangulia mbele ya haki, lengo likiwa ni kukumbuka na kuenzi mchango mkubwa waliotoa katika kujenga msingi wa maendeleo ya taifa. Watanzania wote Bara na Visiwani ni wamoja kiasili, hivyo wanapaswa kushirikiana katika kudumisha misingi iliyoachwa na waasisi wa taifa ili kuweza kujiletea maendeleo.
Aidha Majaliwa aliwaomba Watanzania wote kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja kuulinda na kuudumisha Muungano ulioachwa na waasisi wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere na Shehe Karume.
No comments:
Post a Comment