Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela akizungumza wakati wa kufungua warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa
Meya wa Manispaa ya kinondoni Mheshimiwa Benjamini Sitta ambaye pia ni mwenyekiti wa warsha akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela mara baada ya ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John
Lipesi Kayombo Na Mathias Canal, Dar es salaam akiteta jambo na Meya wa
Manispaa ya kinondoni Mheshimiwa Benjamini Sitta ambaye pia ni mwenyekiti wa
warsha wakati wa warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja
kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural
sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa
katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11,
2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa
Na
Mathias Canal, Iringa
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela
amefungua warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu
programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector
Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika
kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028.
Alisema kuwa ili kukuza na kuendeleza sekta ya kilimo nchini
wataalamu wote nchini wanapaswa kubadilishana ujuzi na kushauriana namna ya
kuwa na kilimo chenya tija kuliko kuficha ujuzi walionao kwa muktadha wa maeneo
husika pekee waliyopo hivyo ni vyema kutumia ujuzi wao kwa makubaliano na
maelekezano kwani jambo hilo litachochea zaidi ukuzaji wa sekta ya kilimo
nchini Tanzania.
Dc Kasesela ameyasema hayo wakati Akizungumza kwenye ufunguzi
wa warsha hiyo inayofanyika katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa, warsha
inayowahusisha Makatibu Tawala wasaidizi upande wa uchumi kutoka mkoa wa Iringa
na Pwani na Maafisa kilimo wa mikoa, Meya wa Manispaa/Wenyeviti wa Halmashauri,
Wakurugenzi wa halmashauri za Manispaa/wilaya, Wachumi wa Manispaa/Wilaya na
Maafisa Kilimo wa Manispaa/Wilaya kutoka Katika Halmashauri za Manispaa na
Wilaya kutoka Mkoa wa Pwani na Dar es salaam.
Dc Kasesela ameeleza kuwa Programu hii ya ASDP 2 imeandaliwa
baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya ASDP 1 iliyotekelezwa kuanzia mwaka
2006/2007 hadi 2013/201 huku akiwapongeza waandaaji wa warsha hiyo ambao ni OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kutaraji kutekelezwa na wadau mbalimbali kama
vile Wizara za sekta ya kilimo, Wahisani, Sekta binafsi, Taasisi zisizo za
kiserikali, Wakulima Wafugaji, na Wavuvi.
Dc Kasesela amesema kuwa Utekelezaji wa ASDP 2 utazingatia
malengo ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano (2016-2021), Mkakati wa Taifa wa
Kilimo, Mifugo na Uvuvi pamoja na Dira ya maendeleo ya Tanzania (2025).
Alisema kuwa Programu hiyo imezingatia vipaombele vya vizara
ya Kilimo, Ufugaji na uvuvi na imelenga kutatua changamoto na kuchochea kasi ya
ukuaji wa sekta ya kilimo, Kuongeza pato la Taifa, Kuboresha kipato cha
wakulima wadogo na usalama wa chakula na lishe nchini.
Sambamba na hayo pia alisema kuwa wadau wote wa ASDP 2
wanapaswa kusimamia na kutekeleza kwa weledi maeneo makuu manne ya utekelezaji
wa Programu hiyo ambayo ni Usimamizi wa Matumizi ya maji na ardhi (Sustainable
Water and Land use Management),, Kuongeza tija na faida katika kilimo, mifugo
na uvuvi (Enhanced Agricultural productivity and profitability).
Maeneo mengine ya kusimamiwa vyema na wadau ni Biashara na
Uongezaji wa thamani kwenye mazao (Commercialization and Value Addition, na
Viwezeshi vya sekta, Uratibu, Ufuatiliaji, na Tathmini ya sekta (Sector
Enablers, Coordination and Monitoring and Evaluation).









0 Comments