Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
Halmashauri
ya Chalinze mkoani Pwani, imepongezwa kwa kuwa ya kwanza nchini kuwalipa wenye
viti wa Vijiji na Vitongoji kutokana na mapato yake ya ndani.
Aidha
Halmashauri za Miji na Majiji nchini zimetakiwa kwenda kujifunza namna ya
ukusanyaji wa mapato kwenye Halmashauri hiyo ambayo inaongoza kwa ukusanyaji
kwenye mkoa huo .
Hayo
yalisemwa Lugoba Chalinze na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi
(UVCCM)Taifa Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa
chama wakati wa ziara yake y'all kukagua uhai wa chama na utekelezaji wa ilani.
Alisema
ametembelea Halmashauri nyingi hapa nchini lakini ameshangazwa na Halmashauri
hiyo kuongoza kwa ukusanyaji wa mapato licha ya kuwa bado changa ikiwa na miezi
nane tu lakini imeongoza kwa kwenye mkoa wa Pwani wenye Halmashauri nane.
"Halmashauri
hii ni ya mfano imeweza kukusanya mapato yake vizuri na kuongoza kwa mkoa na
hata kwa baadhi ya Halmashauri hapa nchini,” alisema Shaka.
Alisema kuwa
kuna Halmashauri kongwe hapa nchini na zinavyanzo vingi vya mapato lakini
havijaweza kuifikia hii ambayo iligawanywa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya
Bagamoyo.
“Huu ni mfano
wa kuigwa na kama mnavyojua Rais Dk John Magufuli amekuwa akihimiza ukusanyaji
wa mapato na kweli wameonyesha njia wengine nao waje kujifunza na haya ndiyo
tunayoyataka ili kuwaletea wananchi maendeleo,” alisema Shaka.
Alieleza
kutokana na mafanikio hayo wameweza sasa kuwalipa posho kila mwezi wenyeviti wa
vijiji na vitongoji jambo ambalo ni zuri na wameweza kuwaondolea wananchi
gharama za mafuta kwa ajili ya kupeleka wagonjwa kwenye hospitali za wilaya na
Tumbi ya rufaa.
“Nimezunguka
maeneo mengi nchini sijasikia kama kuna Halmashauri inawalipa wenyeviti wake wa
Vijiji, Vitongoji na Mitaa hakika nyie mmeweza ,” alisema Shaka.
Alibainisha,
kuwalipa wenyeviti hao kutaondoa ubadhirifu wa mapato ya sehemu husika kwani
ambapo baadhi ya wenyeviti wamejikuta wakiingia kwenye matumizi mabaya ya fedha
za sehemu wanazoongoza.
Awali
mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Said Zikatimu alisema kuwa wao kwa kushirikiana
na madiwani na watendaji waliweka mikakati ya kukusanya mapato ya ndani kwa
asilimia 100 na walifikia malengo hayo.
Zikatimu
alisema bajeti yao kwa sasa imefikia bilioni tatu ambapo wameweza kutoa mikopo
kwa makundi ya vijana na wanawake vikundi 58 na fedha nyingine ziliekezwa
kwenye miradi ya maendeleo.
Akiwa jimbo
la Chalinze Shaka alitemebela miradi ya kisima cha maji kwa shule ya Sekondari
ya Moreto na ujenzi wa kituo cha polisi na kukabidhi mabati na saruji
vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo Ridhiwani Kikwete kwa kata za Halmashauri
hiyo.


0 Comments