wakulima wakionyesha mashamba ya shahiri mkoani Arusha
Safari yenye historia ya kuvutia
ya zao la Shahiri hadi kuwa kinywaji cha bia ya Balimi Extra Lager inaanzia
mbali na eneo la Usukumani ambako ndipo asili ya bia hii ambayo zaidi ya kuwa kinywaji cha kukataa kiu inachangia
kuongeza pato la serikali kubadilisha maisha ya jamii kuwa bora.
Bia ya Balimi inatengenezwa na
kampuni ya TBL Group,iliyopo chini ya kampuni ya kimataifa ya ABin
Bev.Inatengenezwa kwa kutumia malighafi zilizozalishwa nchini Tanzania
ambapo inachangia pato la serikali na
kuchochea maendeleo endelevu kwenye jamii.
Katika wilaya ya Hanang mkoani
Manyara na kwenye mikoa ya Kilimanjaro,Arusha na Njombe wakulima wanapanda
mbegu moja moja ambazo zinawezesha kupatikana mavuno mazuri ya Shahiri
inayotumika kutengeneza bia ya Balimi kwa ubora ikiwa na ladha ya aina yake
inayovutia .
Wakulima ni wawezeshaji wakuu wa
kufanikisha mchakato wa nchi yetu kuelekea katika uchumi wa viwanda.TBL Group
ikiwa inaendesha viwanda vikubwa vya kutengeneza pombe nchini ni moja ya mdau
mkuu wa kuendeleza sekta ya viwanda
ikiwa inafuata mwongozo unaojulikana kama ‘’Dunia Maridhawa ‘’kufanikisha suala hili.
Chini ya mwongozo huu wa ‘Dunia Maridhawa’ itaweza kubadilisha
maisha kwa kila mdau anayechangia kufanikisha utengenezaji wa bia ya Balimi na bia za chapa nyingine zinazotengenezwa na TBL
Group zilizopo kwenye masoko.
TBL Group imekuwa ikishirikiana
na wakulima kwa kuwafundisha mbinu bora za kilimo cha kisasa kuwezesha kupata
mavuno zaidi,pia imekuwa ikiwaunganisha na Shirika la Mpango wa Chakula la
Umoja wa Mataifa kuwawezesha kuuza mazao yao ya ziada kwa bei nzuri pia imekuwa
ikiwaunganisha na mabenki na taasisi nyingine za kifedha kwa ajili ya kupata
mikopo nafuu na huduma nyinginezo za kifedha.
Kupitia ushirikiano huu maisha ya
wakulima zaidi ya 30,000 yamebadilika na kuwa bora zaidi kutokana na shughuli
zao za kilimo ambapo wameweza kuuza malighafi ya kutengenezea Balimi na bia
nyinginezo zinazotengenezwa na TBL Group na kupata faida na kuweza kufanya mambo
mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kujenga mashule,vituo vya afya,kupata maji safi
na kufanya mambo mengineyo mengi ya maendeleo.
Uzalishaji wa bia ya Balimi na
nyinginezo mbali na kuchangia pato la Taifa kwa njia ya kulipa na kukusanya
kodi za serikali pia umewezesha jamii kunufaika kutokana na miradi mbalimbali
inayotekelezwa na TBL Group kuanzia miradi ya kusaidia elimu,kusambaza maji
safi kwa jamii,kampeni za usalama barabarani,na miradi ya afya.
Uhusiano na ushirikiano wa TBL
Group na wakulima mbali na kuwanufaisha
kampuni na wakulima unanufaisha mzunguko wa wadau wetu mbalimbali katika
biashara za kampuni wakiwemo viwanda vya kutengeneza chupa ,wasambazaji wa bia,
mlolongo huu wa wanufaikaji unaenda mpaka kwa watumiaji wa kinywaji cha bia
baridi ya Balimi Extra Lager.
Jina Balimi lina maana ya mkulima
kwa lugha ya Kisukuma moja ya kabila
kubwa katika kanda ya ziwa Victoria ambalo linakishughulisha na Kilimo na
Ufugaji.Kutokana na uhalisia wa mila za kabila hili na maisha yao ya kila
siku,bia ya Balimi imebuniwa kuelezea maisha ya jamii yenye asili ya jina lake
na utamaduni wao.
Balimi ni bia yenye ladha nzuri
na ya kipekee na imetengenezwa kwa maji asili kutoka ziwa Victoria.Chupa yake
nzuri ambayo inaifanya kuwa na mwonekano wa rangi ya jua linalozama unatoa
taswira ya hali halisi ilivyo na watu wanaoishi katika eneo inakotengenezwa.Balimi
inatangazwa uzuri asilia wa maeneo ya kanda ya ziwa Victoria na utamaduni wa
kabila la Wasukuma


0 Comments