Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), tunafahamisha kuwa mechi za mwisho
za Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/2017 zitachezwa kuanzia saa 10.00
jioni bila kujali kama jua linawahi au kuchelewa kuzama.
Muda huo umepangwa ili
kuhakikisha timu zote zinamaliza mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara zinamalizika siku moja ya Mei 20, mwaka huu na kwa muda mmoja,
ikiwa ni pamoja na kudhibiti viashiria vyo vyote vya upangaji wa
matokeo.
Ni jukumu la kila kamishna kuhakikisha mechi anayosimamia inaanza katika muda ulipangwa bila kujali kama kuna mgeni rasmi au la.

0 Comments