Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba
akizungumza wakati wa kikao cha kwanza cha Baraza la Biashara Wilaya
alilozindua rasmi. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa
wa Shinyanga (SHIREMA), Gregory Kibuse).
Wajumbe wa Baraza la Biashara Wilaya ya Kishapu
wakifuatilia kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kishapu, Stephen Magoiga akizungumza katika ufunguzi wa Baraza la Biashara.
Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga, Dk. Meshack
Kulwa akizungumza katika kikao hicho.
Ofisa Biashara Wilaya ya Kishapu, Konisaga Mwafongo
akichangia mada katika kikao hicho.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa
Shinyanga (SHIREMA), Gregory Kibuse akizungumza wakati wa kikao.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa
Shinyanga, Jumbe Samson akifafanua jambo wakati wa kikao.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Shinyanga (SHIREMA), Gregory Kibuse
akitoa maelezo kuhusu shughuli za uchimbaji wa madini aina ya almasi
inayopatikana wilayani Kishapu kwa Mwenyekiti wa Baraza la Biashara, Nyabagnga
Talaba na wajumbe wake.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akiangalia
bidhaa za vigae zilizotengezwa kwa kutumia majani ya mkonge wakati wa maonesho
ya wajasiliamali kabla ya uzinduzi wa Baraza la Biashara Kishapu.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa
Shinyanga (SHIREMA), Gregory Kibuse akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Kishapu,
Nyabaganga Talaba pochi iliyotengezwa kwa mkonge na kikundi cha wanawake wajasiliamali
wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba (kushoto)
akiangalia ngozi ghafi alipotembelea banda la kikundi cha wajasiliamali wa
kutengeneza viatu cha Badimi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela
(kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen
Magoiga wakiangalia viatu vilivyozalishwa na kikundi cha wajasiliamali Cha
Badimi kilichopo wilayani humo.
Mashine ya kupura nafaka zikiwemo mtama iliyobuniwa na
mwananchi wa Kishapu, Daudi Nkende ikiwa katika viwanja vya halmashauri kwa
ajili ya maonesho ya wajasiliamali.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga
Talaba amewataka Watanzania kupenda kununua bidhaa zinazozalishwa hapa nchini
ili kwenda sambamba na sera ya Tanzania yenye viwanda pamoja na kuimarisha
uchumi wetu.
Amesema hayo wakati akizindua Baraza la Biashara Wilaya
ambapo alishangazwa na baadhi ya kuamini kuwa bidhaa zinazozalishwa nchini
hazina ubora na hivyo kukimbilia za nje.
Talaba ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Biashara
Wilaya alisema bidhaa zetu zina ubora kutokana na kutumia malighafi halisi
akitolea mfano viatu vinavyozalishwa na Watanzania ukilinganisha na vinavyotoka
nje ya nchi ambavyo vingi havidumu.
”Tufike mahali sasa tununue bidhaa zetu ili fedha
izunguke kwani tutaimarisha uchumi na kama tunavyofahamu lengo la Rais katika
sera ya nchi ya viwanda anataka tununue bidhaa zetu.
Mkuu huyo wa wilaya alilitaka baraza liwe chachu ya
kusukuma sera ya nchi ya viwanda na kuibua fursa ambazo wananchi waananchi
wanaweza kuzitumia na kuanzisha biashara.
Alilitaka baraza kuja na wazo mbadala la kibishara na kiviwanda
ili wananchi waweze wawaunga mkono wajasirimali wadogo wanaojishughulisha na uzalishaji
wa bidhaa wapate masoko.
Akifungua kikao cha kwanza cha baraza hilo, Mwenyekiti
wa Kamati Tendaji ya Barazaa la Biashara Wilaya, Stephen Magoiga aliwataka
wananchi kutumia vizuri fursa zilizopo wilayani humo.
Magoiga ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri
ya Wilaya ya Kishapu alisema tukitumia vizuri rasilimali zilizopo wilayani humo
tutapiga hatua na kujenga historia.
”Tunapozungumzia viwanda siyo lazima viwe vikubwa hata
vidogo vidogo mfano tunaweza kutumia kilimo kuibadilisha kabisa Kishapu na kuwa
wilaya ya kwanza katika uchumi,” alisema.
Alitaja rasilimali kama madini na fursa za kilimo
zilizopo wilayani humo kuwa kama zikitumika ipasavyo maisha ya wananchi yataboreka
zaidi na uchumi kwa ujumla kuimarika.
Baraza hilo la biashara Wilaya ya Kishapu linaundwa na
wajumbe 40 wakiwemo wawakilishi kutoka sekta ya umma na binafsi na litadumu kwa
kipindi cha miaka mitatu.













0 Comments