Mkaguzi wa ndani wa halmashauri ya Ikungi Kitundu Mkumbo akisoma taarifa
ya ukaguzi mbele ya mkutano maalum wa kijiji cha Ikungi.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akizungumza na wananchi hawapo
pichani kwenye mkutano maalum wa kijiji cha ikungi,kulia kwake ni kaimu
mwenyekiti wa kijiji hicho Athuman Seleman na kushoto kwake ni kaimu
mkurugenzi wa halmashauri Haika Massawe.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ikungi waliohudhuria mkutano maalum wa
kijijji hicho wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu
hayupo pichani.
MKUTANO maalum wa Kijiji cha Ikungi wilayani Ikungi mkoani
Singida umemuondoa Mwenyekiti wa kijiji hicho Hussein Ikusi kutokana na
matumizi mabaya ya madaraka kwa kufanya ubadhirifu wa mali za kijiji
zenye thamani ya shilingi milioni 9.
Ubadhirifu huo aliufanya toka alipoingia madarakani mwaka
2014 akishirikiana na aliyekuwa mtendaji wa kijiji hicho Hamis Isango
aliyehamishiwa kijiji cha Irisya.
Hayo yalibainika baada ya halmashauri ya kijiji kuitisha
kikao maalum tarehe 24 aprili mwaka 2017 wakimtuhumu mwenyekiti kwa hoja
zipatazo 5.
Hoja hizo ni kushindwa kusimamia mali za kijiji,kushindwa
kusimamia mipaka ya kijiji,kushindwa kuonyesha ushirikiano na uongozi wa
halmashauri ya wilaya,Ofisi ya mkuu wa wilaya na taasisi za serikali
zilizopo wilayani,kuwa chanzo cha migogoro badala ya kuwa mtatuzi na
kushindwa kusimamia usomaji wa mapato na matumizi ya kijiji kwa mujibu
wa sheria kwa kipindi cha miaka miwili na nusu.
Ubadhirifu huo umebainishwa na mkaguzi wa mahesabu ya ndani
Kitundu Mkumbo aliyeagizwa na mkuu wa wilaya hiyo Miraji Mtaturu
kufanya ukaguzi wa mapato na matumizi ya kijiji baada ya kupokea tuhuma
kuhusiana na mwenyekiti huyo.
Akizungumza katika kikao cha kutoa taarifa kuhusiana na
maamuzi yaliyoafikiwa na halmashauri ya kijiji Mtaturu alimuagiza kaimu
mkurugenzi wa halmashauri Haika Massawe kumsimamisha kazi mtendaji wa
kijiji cha Irisya Hamis Isango aliyehamishiwa kijiji kingine ili arudi
ikungi kujibu tuhuma za kuondoka na vitabu 12 vya kukusanyia mapato
alivyoshindwa kukabidhi wakati anahama ikiwemo na kutoa maelezo ya
fedha zilizoonekana kupotea mikononi mwake.
"Bwana Ikusi kabidhi fedha na mali kama ushauri wa mkaguzi wa mahesabu alioutoa hapa mbele ya wananchi"alisisitiza Mtaturu.
Aprili 24 mwaka huu halmashauri ya kijiji iliazimia kwa
kauli moja kumuondoa mwenyekiti huyo kutokana na tuhuma hizo dhidi yake
huku huku ikisisitiza kuwa Usimamizi wa Rasilimali za Umma ni
mabadiliko Chanya kwa maendeleo ya Ikungi.




0 Comments