Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani (kulia)
akifafanua jambo wakati akitoa elimu ya mpiga kura kwenye kituo cha redio
Dodoma FM cha mjini Dodoma.Kulia kwake ni Afisa wa Tume Bw. Mawazo Bikenye na
mbeye ni watangazaji .
Hussein Makame-NEC, Dodoma
Tume ya
Taifa ya Uchaguzi imeanza maandalizi ya kufanya uboreshaji wa daftari la kudumu
la wapiga kura kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 baada ya Serikali kutenga
Shilingi Bilioni 10 kwa ajili ya kazi hiyo katika bajeti ya mwaka ujao wa
fedha.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Tume hiyo Bw. Kailima Ramadhani kwa nyakati tofauti
wakati akitoa elimu ya mpiga kura katika vituo vya redio vilivyoko mkoani
Dodoma.
Alisema kuwa
maandalizi ya uboreshaji huo ni pamoja na kutoa elimu ya mpiga kura kupitia
vituo vya redio nchi nzima mpango ambao umeanza kutekelezwa kwa baadhi ya mikoa
nchini.
“Tume imeanza maandalizi ya kufanya uboreshaji
wa daftari la kudumu la wapiga kura, Serikali imeshatenga Shilingi Bilioni 10
kwa ajili ya kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura mwaka 2017/2018”alisema
Bw. Kailima.
Aliongeza
kuwa kwa kipindi hicho Tume itatoa kadi mpya ya mpiga kura kwa
watakaoandikishwa upya, waliopoteza kadi na kadi zilizoharribika, kwa wanaohamisha
taarifa zao ikiwemo waliohamia Dodoma, na kufuta wapiga kura waliopoteza sifa
za kuwa wapiga kura.
Bw. Kailima
aliwataka wananchi wafuatilie elimu ya mpiga kura inayotolewa kupitia redio ya
mikoani kuelewa mambo mbalimbali yanayohusu mchakato wa uchaguzi ili fikapo
mwaka 2020 kila mwananchi awe ameelimika na asiweze kupotoshwa.
Alisema
kwamba kwa muda mrefu elimu ya mpiga kura imekuwa haitolewa kwa mujibu wa
matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria ya Taifa ya
Uchaguzi.
Alifafanua
kuwa Ibara 74 (6) (e) ya Katiba inaitaka Tume kutekeleza majukumu kwa mujibu wa
Sheria nyingine yiyite iliyotungwa na Bunge na Ibara ya 18 inampa kila
mwananchi haki ya kupata taarifa muhimu zinazohusu nchi yake.

0 Comments