Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi ,Vijana ,Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.
Na Daudi
Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali
imesema kuwa haina mpango wowote wa kusitisha mbio za Mwenge wa Uhuru na
kusisitiza kuwa dhana hii ni endelevu na itaendelea kutoka kizazi kimoja hadi
kingine kwa kusisitiza misingi hii bila kuchoka.
Hayo yamesemwa
leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira
na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama wakati akijibu hoja mbalimbali Mjini Dodoma.
“Kutokana na
faida na Mafanikio makubwa yanayopatikana kupitia Mbio za Mwenge wa Uhuru Serikali
inaamini kuwa zipo faida nyingi ndani yake na mwenge huu utaendelea kudumu”,Alisisitiza
Mhe.Muhagama.
Amesema kuwa
Kimataifa Mwenge wa Uhuru umeendelea kusimamia dhana na maudhui yake ya
kumulika hata nje ya mipaka yetu kwa kuwa msuluhishi wa Amani Afrika na mfano
wa kuigwa kwa mataifa mengine Afrika na Dunia kote.
Aidha
amesisitiza kuwa Umoja ,Mshikamano ,Upendo na Ukarimu wa Watanzania ni matunda ya Mwenge wa Uhuru.
Mhe.Muhagama
ametoa takwimu ambazo zinaonyesha kuwa Miradi ya Maendeleo iliyozinduliwa
pamoja na kuwekewa mawe ya msingi kupitia Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2015 ni
miradi 1342 yenye thamani ya bilioni 463,519,966,467.
Pamoja na hayo
amezitaja faida za Mwenge wa Uhuru kuwa ni kuendelea kuamasisha ari ya wananchi
kujitegemea na kuwekeza katika maeneo mbalimbali katika Taifa letu,pia kimekuwa
ni chombo pekee cha kujenga umoja na mshikamano na kudumisha amani pale
unapopita bila kujihusisha na itikadi za kisiasa.
Aidha Mwenge
wa Uhuru umeendelea kuhamasisha na kuimarisha umuhimu wa Muungano kwa
Watanzania wa pande mbili za nchi yetu na kila mwaka huweka mawe ya msingi
kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi na kuhamasisha uzalendo wa
kuendelea kujitolea.

0 Comments