TAARIFA KWA UMMA
UTARATIBU MPYA WA UWASILISHAJI
WA MICHANGO NA MALIPO MENGINEYO KWA WAAJIRI NA WANACHAMA WA MFUKO WA TAIFA WA
BIMA YA AFYA (NHIF)
Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umefanya maboresho ya uimarishaji wa mfumo wa
uwasilishaji wa michango na malipo ya huduma nyinginezo kutoka kwa waajiri na
wanachama wake kupitia benki.
Kutokana
na maboresho hayo, kuanzia tarehe 1 Juni
2017, mwajiri au mwanachama anatakiwa kuwa na namba rejea ya malipo
(payment reference number) kila anapowasilisha michango au kufanya malipo
kupitia tawi lolote la benki ya NMB.
Ili
kupata namba rejea ya malipo, waajiri na wanachama wanatakiwa kutekeleza
utaratibu ufuatao:
- Mwajiri
anatakiwa kutumia mfumo wa mtandao unaopatikana kupitia anuani https://verification.nhif.or.tz/serviceportal
na kufuata maelekezo hatua kwa hatua. Maelekezo kamili ya namna ya kutumia
mfumo huo yanaweza kupakuliwa kwa kubonyeza eneo lililoandikwa “Download”;
- Pamoja
na mfumo huo, mwanachama anaweza pia kutumia simu ya mkononi kwa kupiga
namba *152*00# na kufuata
maelekezo. Huduma hii inapatikana kupitia mitandao ya Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel tu.
- Nukuu
namba rejea ya malipo na kuitumia wakati wa kufanya malipo halisi (actual
payment) kwenye benki ya NMB
kupitia njia zake mbalimbali za ukusanyaji fedha (cash collection
channels) ikiwemo njia ya simu za mkononi (mobile payment), kaunta za
matawi ya benki hiyo n.k.
Kwa msaada zaidi tafadhali wasiliana
na kituo cha huduma kwa wateja kwa
kupiga simu namba 0800 110063
(bila malipo).
Imetolewa
na;
KAIMU
MKURUGENZI MKUU
Mei 2, 2017
0 Comments