Ndugu zangu viongozi, wapenzi na wadau wa mpira wa miguu Tanzania.
Kama ilivyotangazwa na kamati yetu ya uchaguzi leo tumeanza rasmi mchakato wa uchaguzi wetu.
Hiki ni kipindi muhimu kwa ustawi wa mpira wetu.
Ninaomba niwahakikishie wadau wa
mpira wa miguu Tanzania kuwa Sekretarieti ya TFF ambayo kikatiba
ninaisimamia mimi itaendelea na shughuli zake bila kuathiriwa na
mchakato huu, hii itakuwa ni pamoja na kuandaa timu zetu mbalimbali za
Taifa na kushughulikia majukumu yake mengine ya kila siku.
Aidha ninaomba niwahakikishie
viongozi na wadau wa mpira wa miguu Tanzania kuwa mimi kama Rais wa TFF
sina kundi katika uchaguzi huu.
Msimamo wangu ni kuwa wagombea
wote wana haki sawa na sanduku la kura ndilo litaamua nani ataongoza
mpira wetu kwa kipindi cha 2017-2021.
Wagombea wote ninawatakia kila la kheri na Mola awabariki na kuwaongoza.
Ahsanteni
Jamal Emil Malinzi
Rais wa TFF
.……………………………………………………………………………………………..
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

0 Comments