Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akizungumza
pale ugeni kutoka Umoja wa Wanamichezo wa Mpira wa Miguu kutoka FC GRACE UNITED
STATES ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. wa pili kulia ni Mwenyeji
na kiongozi wa Msafara Bishop Oscar John.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati)
akimsikiliza Mheshimiwa William Ngeleja akizungumza wakati Umoja wa Wanamichezo
wa Mpira wa Miguu kutoka FC GRACE UNITED STATES ulipomtembelea leo Ofisini
kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa tatu
kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Washindi wa Medali za Dhahabu katika
Mashindano ya kimataifa ya Mazingira na Sayansi yaliyofanyika hivi karibuni nchini
Marekani. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shule ya Wavulana ya Feza Ndg.
Ibrahim Rashid, anaefuata ni Ndg. Rashid Kikwete, kulia ni Mhe. Hawa Ghasia, wa
pili kulia ni Ndg. Kassi Nkamia na watatu kulia ni Ndg. Abdallah Rubeya,
waliotembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akimsikiliza
Bishop Oscar John (aliesimama) akizungumza, pale ugeni kutoka Umoja wa
Wanamichezo wa Mpira wa Miguu kutoka FC GRACE UNITED STATES ulipomtembelea leo Ofisini
kwake Mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson
(katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Chama cha
Msalaba Mwekundu Tanzania ulioongozwa na Rais wa Chama hicho Ndg. Mwadini Jecha
(kushoto waliokaa) baada ya kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini
Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson
(kulia) akimsikiliza Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania Ndg. Mwadini Jecha (katikati) pale ugeni
kutoka Chama hicho ulipomtembelea leo
Ofisini kwake Mjini Dodoma, kushoto ni Mratibu wa Mawasiliano Ndg. Anne kilimo.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia)
akizungumza na ugeni kutoka Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania ulioongozwa na
Rais wa Chama hicho Ndg. Mwadini Jecha (katikati) na Mratibu wa Mawasiliano
Ndg. Anne kilimo (kushoto) uliomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.





0 Comments