Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) aimewafikisha katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wafanyabiashara James Rugemarila na
Harbinder Sethi kwa tuhuma za uhujumu uchumi na makosa mengine
yanayofanana na hao.
Hayo
yamesemwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Valentino Mlowola
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa muda
mrefu wamekuwa wakiulizwa kuhusu kesi ya Escrow hivyo sasa anaamini ni
wakati muafaka wa kuwafikisha watuhumiwa hao wawili mahakamani.
Mlowola
alisema kuwa taasisi hiyo imefanya uchunguzi wa kutosha kwa muda wote
ambao ilikuwa kimya, na hivyo wamefikishwa mahakamani kisutu na baada ya
hapo mahakama itafanya taratibu za kuhamishia kesi hiyo katika Mahakama
ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Kabla
ya vigogo hawa wawili kufikishwa mahakamani leo, baadhi ya watumishi wa
TANESCO tayari walishtakiwa kufuatia tuhuma za kupokea fedha kutoka kwa
Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engeneering & Marketing ambaye pia
alikuwa Mkurugenzi wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power
Tanzania Ltd (IPTL), James Rugemalira.


0 Comments