Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akiongea na wadau mbalimbali wa
sekta ya Afya wakati wa uzinduzi wa huduma ya kupandikiza kifaa cha usikivu kwa
watoto wenye matatizo ya kusikia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo
jijini Dar es salaam kulia ni Mwenyekiti wa Bodi wa Muhimbili Prof.Charles
Majinge.
Picha Na Ally Daud-WAMJW Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili kushoto akiongea na wadau mbalimbali wa sekta ya Afya wakati
wa uzinduzi wa huduma ya kupandikiza kifaa cha usikivu kwa watoto wenye
matatizo ya kusikia katika Hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam katikati ni
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na
kulia ni Mwenyekiti wa Bodi wa Muhimbili Prof.Charles Majinge.
Wadau mbalimbali wa sekta ya Afya na waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu hayupo pichani
wakati wa uzinduzi wa huduma ya kupandikiza kifaa cha usikivu kwa watoto wenye
matatizo ya kusikia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo jijini Dar es
salaam
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akimsalimia mlezi Theodora Myalla
aliyembeba mtoto Meckzedeck Kibona (2)
mkazi wa Tegeta aliyepandikizwa kifaa cha usikivu wakati alipozindua huduma
hiyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akifurahia jambo na baadhi ya
watoto waliopandikizwa vifaa vya usikivu wakati wa uzinduzi wa huduma ya
kupandikiza kifaa cha usikivu kwa watoto wenye matatizo ya kusikia katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo jijini Dar es salaam.
....
NA WAMJW-DAR ES SALAAM.
WATOTO wenye matatizo ya usikivu watapata
matibabu ya kupandikizwa vifaa vya
usikivu hapa nchini katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili badala ya kwenda nje
ya nchi kwa matibabu kama ilivyokuwa awali.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.
Ummy Mwalimu wakati alipozindua huduma hiyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
leo jijini Dar es salaam.
“Serikali
haitapeleka mgonjwa mwenye matatizo ya kusikia nje ya nchi kwa ajili ya
kupandikizwa vifaa vya kusikia na badala yake atatibiwa nchini ili kupunguza
rufaa za wagonjwa wan je ya nchi” alisema Mh. Ummy.
Aidha
Waziri Ummy amesisitiza juu ya umuhimu
wakujiunga na mfuko wa Afya wa Jamii wa NHIF ili kupata fursa ya kutibiwa kwa
gharama ndogo zaidi, huku akisisitiza kuwa wananchi wote watakaokuwa na kadi ya
NHIF wataweza kupata matibabu ya upandikizaji wa kifaa cha kusikia bure kupata
huduma hii.
Mbali na hayo Mh. Ummy ameahidi kuwa Serikali kupitia Wizara yake ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuunga mkono kwa kuisaidia
hospitali ya Muhimbili ili kuendelea kufanikisha upasuaji wa Watoto hivyo
kupunguza gharama inayopata Serikali kusafirisha Watoto hao nje ya nchi pindi
wapatapo matatizo hayo.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali ya Muhimbili Lawlence Mseru amsisitiza kuwa moja kati ya mipango
ya Hospitali ya Muhimbili ni kuhakikisha kuwa wanapunguza idadi ya
wagonjwa wanaokwenda kutibiwa nje ya nchi kila mara jambo linaloigharimu
Serikali pesa nyingi.
Aidha
Dkt. Mseru aliongeza kuwa licha ya kufanikisha tukio hilo la Kihistoria wanaomba Serikali kupitia Wizara ya Afya
kusaidia kuboresha Wodi za Wagonjwa mahututi, ununuzi wa Vifaa tiba, kuongeza
vyumba vya upasuaji jambo litalopunguza msongamano wa shughuli za hospitali pia kuongeza
Wataalamu waendao nje ya nchi kwaajili ya mafunzo ili kuendeleza huduma katika
nchi yetu jambo litakalosaidia kuwa na Wataalamu wengi hivyo kuweza kufanikisha
huduma kwa wagonjwa wengi zaidi.
Nae Prof. Sunil Narayan Dutt kutoka Hospitali ya
Apollo nchini India ameipongeza Serikali
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa
jitihada inayoonesha hasa katika kutetea haki za watoto.
Kwa
upande Bi. Hilda Bohela ambae ni mzazi wa Apulie Bohela aliyepata huduma hiyo
nchini amewasihi wazazi wenzie kuwapeleka
watoto kufanyiwa uchunguzi pindi waonapo hali isiyokuwa yakawaida kwa watoto
wao na kuachana na mila potofu jambo linalopelekea watoto wengi kupata ulemavu .






0 Comments