Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati waliokaa) akishiriki mazoezi ya Yoga katika maadhimisho ya Mchezo huo hapa nchini yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
Na Shamimu Nyaki –
WHUSM.
Wadau wa mchezo wa Yoga
nchini wametakiwa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi ili wapate kuufahamu na
kushiriki kwa ajili ya kuimarisha afya zao na kuongeza ufanisi katika kazi zao za kila siku .
Hayo yamesemwa na
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harisson Mwakyembe wakati
wa maadhimisho ya siku ya Yoga jana Jijini Dar es Salaam katika uwanja wa uhuru.
“Nimefarijika kuwa
sehemu ya maadhimisho haya kwani nilikuwa nafikiri Yoga ni mchezo wa misuli tu
lakini leo nimejionea mwenyewe uhalisia wake na jinsi unavyounganisha akili na
mwili kwa pamoja, nawaomba muelimishe wananchi mchezo huu ili nao waweze
kushiriki.” Alisema Mhe. Mwakyembe.
Aidha Mhe. Mwakyembe
amewashauri waandaaji wa mchezo huo kuupeleka Mkoani Dodoma ambapo ndipo makao
makuu ya nchi ili kuwapa fursa viongozi wa Serikali na Wabunge kushiriki kwa
manufaa ya afya na kuongeza utendaji kazi.
Kwa upande wake Balozi
wa India hapa nchini Mhe. Sandeep Arya amesema kuwa Serikali yake itatekeleza
ombi la Mhe. Waziri Mwakyembe la kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mchezo huo ili
kuendeleza ushirikiano baina ya nchi hizo.
Mchezo wa Yoga ni
mchezo wa kuchezesha viungo vya mwili lengo lake likiwa ni kuimarisha afya ana
akili na huadhimishwa Juni 18 kila mwaka.

0 Comments