Viongozi na Waumini ya Dini ya Kiislam mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye sala ya magharibi wakati Iftar maalum iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye makazi yake
Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Raia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wakisoma Qasida kwenye Iftar maalum
iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimkabidhi cheti cha shukrani Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa
Clouds Media Group Bw. Ruge Mutahaba kwa ushiriki na ufanikishaji wa
maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa ilifanyika
Butiama.
Wengine waliopokea vyeti hivyo ni TBC, Lake Gas, TBL, WWF na ZANTAS.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akimkabidhi cheti cha shukrani Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL,Roberto Jarrin kwa ushiriki na
ufanikishaji wa maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa
ilifanyika Butiama.
Wengine waliopokea vyeti hivyo ni TBC, Lake Gas, Clouds Media, WWF na ZANTAS.
Ndugu, Jamaa, Marafiki na Wadau kutoka sekta mbali mbali wakipata futari kwenye
Iftar maalum iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye makazi yake
Oysterbay jijini Dar es Salaam.





0 Comments