Kamishna Jenerali wa Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimkabidhi zawadi Balozi wa Kuwait
nchini, Jasem Al-Najem (kushoto), baada ya mazungumzo na Balozi huyo
alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo, jjini Dar es Salaam leo. Katika Kikao
hicho Balozi huyo aliahidi kushirikiana na Jeshi kubadilishana utaalamu katika
masuala ya kukabiliana na majanga mbalimbali.
Kamishna Jenerali wa Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akizungumza na Balozi wa Kuwait
nchini, Jasem Al-Najem (Wakwanza kulia) alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo
jijini Dar es Salaam leo. Katika Kikao hicho Balozi huyo aliahidi kushirikiana
na Jeshi hilo kubadilishana utaalamu katika masuala ya kukabiliana na majanga
mbalimbali. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo.
Balozi wa Kuwait nchini,
Jasem Al-Najem, akizungumza wakati wa kikao na Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye (katikati) na Maafisa Waandamizi wa
Jeshi hilo, alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi jijini Dar es Salaam leo.
Katika Kikao hicho Balozi huyo aliahidi kushirikiana na Jeshi hilo
kubadilishana utaalamu katika masuala ya kukabiliana na majanga mbalimbali.
Kamishna Jenerali wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akiongozana na
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem (kulia) alipowasili Makao
Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam leo kwa mazungumzo yaliyohusisha
ushirikiano kati ya Majeshi ya nchi hizo kubadilishana Utaalamu katika masuala
ya kukabiliana na majanga mbalimbali.
Kamishna Jenerali wa Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akiwa katika picha ya pamoja
na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem (katikati) baada
ya kikao cha mazungumzo yaliyohusisha ushirikiano kati ya Majeshi
ya nchi hizo katika kubadilishana Utaalamu katika masuala ya kukabiliana
na majanga mbalimbali.
....................................
Na
Mwandishi Wetu
Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Nchini, liko katika mkakati wa kuingia ushirikiano na
Serikali ya Kuwait katika shughuli zake za kukabiliana na majanga ya moto ikiwa
ni juhudi zake katika kuyafikia maeneo mengi nchini.
Akizungumza
alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dar es salaam,
Balozi wa Kuwait Nchini, Jasem Al-Najem, alisema serikali ya Kuwait ipo tayari
kubadilishana mafunzo na kutoa msaada wa vifaa kwa Jeshi hilo.
“Ni vema
tukatengeneza mpango ambao wataalam wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
kutoka nchini Tanzania wataweza kubadilishana uzoefu na wataalamu
kutoka nchini Kuwait kwa ajili ya kujifunza mbinu mbalimbali za kukabiliana na
majanga pindi yanapotokea, ’’ Alisema Balozi huyo.
Akizungumza
wakati wa kikao hicho, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,
Thobias Andengenye alimshukuru kwa kumtembelea na kusema kuwa ujio wa balozi
huyo, umefungua ukurasa mpya kwa upande wa misaada na mafunzo kwa Askari wa
Jeshi hilo, kwani watapata fursa ya kubadilishana uzoefu na kuongeza tija kwa
Jeshi lake.
“Tutapata
nafasi ya kubadilishana uzoefu na kupata mafunzo kutoka Nchi ya Kuwait na
kuongeza ufanisi katika majukumu yetu ya kila siku, lengo ikiwa ni kukabiliana
na majanga mbalimbali yakiwemo ya moto,’’ alisema Kamishna Jenerali.
Katika kikao
hicho Balozi wa Kuwait, Nasem Al-Najem alipokea taarifa ya changamoto
zinazolikabili jeshi hilo ikiwemo uhaba wa vitendea kazi huku akiahidi
kuzifanyia kazi na akisisitiza mchakato wa kusaini makubaliano ya hiari
ukamilike kwani utakuwa msaada wa kutekeleza kwa haraka program za
mafunzo ya muda mfupi.





0 Comments