Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa Water Aid Tanzania kwa
mwaka 2016-2021 wenye kauli mbiu "Kuweka Maji na Usafi wa Mazingira kuwa
kitovu cha Maendeleo"iliyofanyika kwenye hotel ya HyattRegency jijini
Dar es Salaam.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akionyesha kitabu maalumu chenye mpango mkakati wa Water Aid uliozinduliwa kwenye kwenye hotel ya HyattRegency jijini
Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson
Lwenge wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa Water Aid Tanzania kwa
mwaka 2016-2021 wenye kauli mbiu "Kuweka Maji na Usafi wa Mazingira kuwa
kitovu cha Maendeleo"iliyofanyika kwenye hotel ya HyattRegency jijini
Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mohamoud Thabit
Kombo wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa Water Aid Tanzania kwa
mwaka 2016-2021 wenye kauli mbiu "Kuweka Maji na Usafi wa Mazingira kuwa
kitovu cha Maendeleo"iliyofanyika kwenye hotel ya HyattRegency jijini
Dar es Salaam.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
..........
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassana leo amezindua Mpango Mkakati wa Water AID Tanzania .
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt
Regency jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji
Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge, Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit
Kombo, Mkurugenzi wa Water Aid Kanda ya Afrika Mashariki Bi. Olutayo Bankole –Bolawole,Mkurugenzi
WaterAid Tanzania Dkt. Ibrahim Kabole na wadau mbali mbali wa maji, afya na
mazingira.
Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Water Aid Tanzania wenye
lengo la “ Kuweka Maji Safi na Usafi wa Mazingira (WASH)” katika mipango ya
Maendeleo ya Jamii.
Makamu wa Rais aliwapongeza
Water Aid Tanzania kwa mpango wake huo, alisema Maji ni rasilimali ambayo
haijawahi kutosheleza mahitaji ya dunia
na hapa kwetu pia kwani kuna mahitaji makubwa ya maji kwa ajili ya shughuli za
kijamii, kiuchumi na kuhuisha na kutunza mazingira.
Vilevile vyanzo vya
maji vinaathiriwa sana na Ukame,kufurika n, kuvuruga mtiririko asilia,
mabadiliko ya hali ya hewa ongezeko la idadi ya watu na viumbe wengine
(Wanyama).
Mpango wa Water Aid Tanzania wa miaka mitano utawezesha kuiweka Tanzania kwenye ramani ya
matumizi endelevu ya rasilimali ya maji na utachangia katika utekelezaji wa
malengo tuliyojiweka ya kupeleka huduma ya maji safi na salama kwa wananchi
kulingana na Sera yetu ya Maji na pia kutekeleza ahadi tulizozitoa kwenye Ilani
ya Uchaguzi ya 2015.
Makamu wa Rais alisema Serikali kwa kushirikiana na wadau
mbali mbali imeendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na
salama katika maeneo ya vijijini ambapo utekelezaji huo umeendelea kuboresha
hali ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini ambapo kwa mwezi Juni 2017 jumla
ya watu 22,952,371 sawa na asilimia 72.58 ya wananchi waishio vijijini wanapata
maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kama sera ya maji ya mwaka 2002
inavyoelekeza huku katika Miji Mikuu ya
mikoa kutoka asilimia 86 hadi asilimia 95, katika miji mikuu ya Wilaya , miji
midogo na miradi ya Kitaifa kutoka asilimia 60 hadi asilimia 75 na katika jiji
la Dar es Salaam kutoka asilimia 72 hadi asilimia 95 ifikikapo 2020.
Makamu wa Rais alisisitiza suala la usafi wa mazingira na
kuhakikisha tunalinda afya zetu tusishambuliwe na magonjwa ya milipuko
kama vile kipindu pindu na homa za
matumbo. “Sote tunajukumu kubwa
kuhakikisha tunapata maji na kuzungukwa na Mazingira safi”.
Makamu wa Rais aliwaagiza wanaohusika na usimamizi wa miradi
ya maji na usafi wa mazingira kuongeza jitihada zaidi ifikapo 2020 idadi ya
wananchi wanaopata maji iwe imeongezeka kufikia malengo tuliyojiwekea.
Mwisho, Makamu wa Rais aliwashukuru wawakilishi wa mashirika
yote ya Maendeleo, wafadhili binafsi na Watendaji wengine ikiwa pamoja na Sekta
Binafsi na Taasisi za Kidini ambazo zimesaidia katika upatikanaji wa huduma za
maji na usafi wa mazingira na kuboresha mazingira.




0 Comments